Mhe. Balozi Mulamula akiingia ukumbini kwenye sherehe ya kumkaribisha rasmi nchini Marekani iliyoandaliwa na jumuiya ya Watanzania DMV siku ya Jumamosi  Novemba 9, 2013 Lanham, Maryland na kuhudhuriwa na Watanzania kutoka majimbo mbalimbali wakiwemo viongozi wa jumuiya ya New York.
Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV bwn. Idd Sandaly akiongea na Watanzania na marafiki zao waliofika kwenye sherehe ya kumkaribisha rasmi Balozi Mulamula siku ya jumamosi Novemba 9, 2013 iliyofanyika Lanham, Maryland, machache aliyoongea Rais wa jumuiya ni msisitizo wa Watanzania DMV kujiunga na jumuiya kwani umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu na baadae alimkaribisha Mhe. Balozi Liberata Mulamula.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akicheza wimbo huku akisindikizwa na wakina mama na watoto wa darasa la kiswahili DMV wakati alipokua akielekea kuongea na Watanzania waliofika kumsikiliza.
Juu na chini ni Balozi Liberata Mulamula akiongea na Watanzania DMV siku ya Jumamosi Novemba 9, 2013 Lanham, Maryland pamoja na mambo mengi aliyoongea hotuba yake iliwasisimua wengi kiasi cha kumshangilia kwa wimbo wa "Balozi sema, sema usiogope sema" alianza kwa kumsifia Balozi aliyepita Mhe. Mwanaidi Maajar kwamba amevaa viatu vyake ambavyo kwake yeye ni vikubwa na aliwaasa Watanzania kujiunga na jumuiya za Wanzania na kusisitiza wasigawanyike kwa msingi ya tofauti zao za dini, itikadi au rangi na kuwaomba viongozi wa jumuiya kuwa wabunifu wa mambo ya msingi ambayo yanamanufaa kwa Mtanzania aishiye ughaibuni akatoa mfano wa Bima ya maisha na maswala ya uhamiaji huku akisisitiza kwa kusema tusiwe wachoyo wakupeana siri za mafanikio ya mambo yenye manufaa na yatakayomsaidia Mtanznia mwenzako, kama wewe 
Juu na chini ni Watanzania na marafiki zao wakimsikiliza mhe. Balozi wakati alipokua akiongea na Watanzania kwenye sherehe ya kumkaribisha rasmi iliyoandaliwa na jumuiya ya Watanzania DMV.
Juu na chini Balozi Liberata Mulamula akipongezwa kwa hotuba yake nzuriiliyowagusa wengi aliyotoa kwenye sherehe ya kumkaribisha rasmi iliyoandaliwa na jumuiya ya Watanzania DMV.
kwa picha zaidi bofya HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Marekani imepata Jembe lingine.UK mpooooooo? Mbona hamsikiki? Kimyaaaa.

    ReplyDelete
  2. Nimependa sherehe za huko, hapa nyumbani hizo mez zingechafuka utafikiri hapatakua na mnuso mwingine karibuni.

    ReplyDelete
  3. Tatizo uk hakuna umoja, kuna makundi tu kama ccm,cdm,cuf na mipasho tu mchana na usiku kwenye line za simu za bure. Uitaka kuona ukweli huo angalia wanapokuja viongozi uk sura utazoziona ubalozini ni zilezile zinazowakilisha chama Fulani kwa kweli tupo ovyo sana balozi anajitahidi sisi wenyewe ndio tuna muangusha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...