Familia ya marehemu Bw. Elifadhili Mkaze Mnzava wa Chang’ombe, Temeke, Dar Es Salaam wanatoa shukrani za dhati kwa ndugu, jamaa, na marafiki walioshiriki katika kumuuguza mpendwa wao hadi alipoitwa na Bwana tarehe 14/10/2013 usiku na kuzikwa tarehe 18/10/2013.

Tumeguswa sana kwa faraja mliotupa katika kipindi kugumu cha majonzi. Mmetuonyesha moyo wa kujali na upendo wa kipekee. Sio rahisi kumshukuru mtu mmoja mmoja, hivyo tunaomba mpokee shukrani zetu za jumla. Ila shukrani za pekee ziwafikie Viongozi wa Serikali na wafanyakazi wote wa:

Wizara ya Maliasili na Utalii;
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa;
Taasisi ya Teknolojia Dar Es Salaam (DIT);
Kampuni ya Radar Recruitment;
Tume ya Taifa ya UNESCO;
Madaktari na Wauguzi wa Hospitali za Hindul Mandal, TMJ (DSM), Hospitali ya Taifa ya Muhimbili; Hospitali ya Apolo (Delhi India) na Hospitali ya Nairobi (Kenya), Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) na Surgi Pharmacy(DSM).
Mchungaji Kiongozi na waumini wa Kanisa la K.K.K.T- Usharika wa Temeke (Wailes) ;

Aidha, tunawashukuru majirani wa Chang’ombe na Kijitonyama kwa ushirikiano wao waliotupa katika kipindi chote cha msiba. Ni dhahiri sisi wenyewe tusingeweza, lakini kwa Neema mmetuwezesha. Mbarikiwe!

Karibuni katika Ibada ya shukrani itakayofanyika katika Kanisa la K.K.K.T Usharika wa Temeke (Wailes), Jumapili ya tarehe 17/11/2013, saa 1 asubuhi.

‘Maana wao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza’

1 Wathesalonike 4:14-17

MUNGU AWABARIKI WOTE.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Pumzika kwa amani Baba. We will miss you.

    ReplyDelete
  2. Ernest Mnzava - NDCNovember 15, 2013

    Nawapa pole familia yote kwa ujumla na Mungu ailaze mahali pema Roho ya Marehemu Mzee E. Mnzava.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...