FAMILIA YA BWANA NATHAN
MSHANA WA VUDEE MSANGA, SAME, KILIMANJARO, TUNAPENDA KUTOA SHUKRANI NYINGI NA
ZA DHATI KWA WOTE MLIOKUWA NA SISI MUDA WOTE WAKATI WA KUMUUGUZA MTOTO WETU
MPENDWA JANE NATHAN HADI PALE BWANA ALIPOMWITA KATIKA NYUMBA YA MILELE TAREHE 31/10/2013
NA KUZIKWA TAREHE 3/11/2013 NYUMBANI VUDEE MSANGA, WILAYA YA SAME.
SHUKRANI ZIWAENDEE MADAKTARI NA
WAUGUZI WOTE WA HOSPITALI YA MOUNT MERU ARUSHA WALIOMUUGUZA MPAKA SIKU YA MAUTI
YAKE; MADAKTARI NA WAUGUZI WA HOSPITALI ZA REGENCY, AGA KHAN, SELIAN ARUSHA NA
HOSPITALI YA RUFAA MUHIMBILI AMBAO WALIMUUGUZA KWA MIDA TOFAUTI TANGIA MWEZI
SEPTEMBA 2012.
SHUKRANI ZA PEKEE ZIWAENDEE UTAWALA
NA WAFANYAKAZI WA BENKI YA CRDB ARUSHA; AAR INSURANCE; WAFANYAKAZI WA
HALIMASHAURI ZA WILAYA ZA MISUNGWI, KARATU, ARUSHA, MBULU NA MWANGA; KANISA LA
KILUTHERI USHARIKA WA MKANYENI VUDEE SAME; WANANCHI WOTE WA VUDEE MSANGA,
NDUGU, JAMAA, MAJIRANI NA MARAFIKI WOTE WALIOSHIRIKIANA NASI KUFANIKISHA MAZISHI
YA MTOTO WETU.
ASANTE
NA BWANA WABARIKI
“BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA,
JINA LAKE LIHIMIDIWE”, AMEN
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...