JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
 WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Maswali mengi yanaulizwa kuhusu uraia, hasa wakati huu ambapo zoezi la kuwabaini wageni wanaoishi nchini kinyume cha sheria linaendelea katika maeneo mbalimbali nchini, yakitaka kujua nani hasa ni raia wa Tanzania. 

Kimsingi, masuala ya uraia duniani kote yanaongozwa na falsafa kuu mbili ambazo ni Haki za Kidamu (Jus Sanguinis - The rights of blood), ambapo mtu hupata uraia kutokana na uhusiano wa kidamu na wazazi wenye uraia wa nchi husika. Hii ina maana kwamba, pamoja na mtu kuzaliwa katika nchi husika anatakiwa pia kuwa na mzazi ambaye ni raia wa nchi hiyo. Falsafa hii ndiyo inayofuatwa na nchi ya Tanzania. 

Kwa maana nyingine kuzaliwa pekee nchini Tanzania hakumpi mtu haki ya moja kwa moja ya  kuwa raia wa Tanzania, bali mtu atakuwa raia ikiwa amezaliwa Tanzania na wakati wa kuzaliwa kwake mzazi wake mmoja sharti awe ni raia wa Tanzania.

Falsafa nyingine ni (Jus Soli - The right of Soil), ambayo mtu  hupata Uraia kutokana na kuzaliwa kwake katika ardhi ya nchi fulani. Kufuatana na Falsafa hii, mtu hupata uraia kutokana na kuzaliwa katika nchi husika bila kujali uraia wa wazazi wake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Bado Vigezo viwili vya Uraia wa Tanzania ni tata:

    1.Jus-Sungunis/DAMU
    2.Jus-Solis/ARDHI

    Je Uraia wa mmoja wa wazazi wawili wa muhusika utathibitika vipi?

    Tukisema Uraia wa mmojawapo wa wazazi kuwepo ndani ya nchi iliyokuwa initwa Tanganyika kabla ya tarehe 9 Desemba 1961 ,ama Zanzibar kabla ya 12 Januari 1964 ama kabla ya tarehe 26 Aprili 1964.

    Mfano Wapo Wanyarwanda walifika Tanzania mwaka 1959 (YAANI KABLA YA UHURU WA TANGANYIKA)...TUNAOMBA MAELEZO TAFADHALI.

    Je hapo itakuwaje?

    ReplyDelete
  2. ANAYEZALIWA TANZANIA NA MZAZI AMBAYE SI RAIA INAMAANA NI MHAMIAJI HARAMU NA INABIDI AKAMATWE MARA TU ANAPOZALIWA? HIKI NI KIROJA CHA MATOKEO MAKUBWA SASA, NA NINA UHAKIKA HAKUNA NCHI ITAKAYOKUWA TAYARI KUMPOKEA KWANI HANA PASI YA KUSAFIRIA PIA HAKUNA USHAHIDI KUWA ALITOKA KWENYE NCHI INAYOTAKIWA KUMPOKEA.

    ReplyDelete
  3. Wagogo na wachaga Tu

    ReplyDelete
  4. Hahahaha Mdau wa Pili, ama kweli hayo aajabu ya MATOKEO MAKUBWA SASA, yaani BIG RESULTS NOW (BRN).

    Kwa kweli kwa msimmo huo hakuna atakaye pona na Operesheni Kimbunga hata Mjomba Michuzi atajikuta anasukumiwa Bujumbura-Burundi na huku Mhe. Dr. Nchimbi akibaki na Mhe. Raisi JK peke yao wakiwa wao ndio wa-Tanzania wa kweli !!!

    ReplyDelete
  5. Mdau wa nne 4 juu.

    Hahahaha baada ya Mjomba Michuzi kubebwa na Kimbunga,

    Itabidi Wadau wa Libeneke tupitishe Bakuli kwa Makapu Makanisani na Kofia Misikitini ili kuchangisha nauli ya kumtumia Mjomba Michuzi Bujumbura-Burundi arudi Tanzania!

    ReplyDelete
  6. heheheheh

    Ankali Michuzi baada ya kubwagiwa Burundi na Operesheni Kimbunga tutakupa Mchongo mpya wa kuingia tena Bongo!

    Tutakununulia Birika uifika tu Tanzania uwe Muuza Kahawa!!!

    ReplyDelete
  7. Ohooo !

    Hii Sheria ya Uraia imekaa Kimtego sana, ni kuwa ikitokea mtu akikukalia vibaya anaweza kukujengea hoja ukaitwa Mhamiaji Haramu na makubwa yakakukuta.

    ReplyDelete
  8. Serikali iache kubabaisha watu bali ifanye maamuzi magumu ya hili swala. Mie naona iseme tu kama inatoa uraia pacha au hapana, yote shega tu. Viongozi wetu wanajikanyaga kanyaga sana mpaka wanaboa. Na watu watawachagua hao hao. Uchaguzi unaokuja nipo tayari kuchagua viongozi na kuwanadi viongozi wale wenye moyo wa kupenda maendeleo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...