Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya makubaliano ya kukabidhi Mgodi wa Tulawaka kwa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), kutoka kwa kampuni ya uchimbaji wa madini ya African Barrick Gold (ABG), katika hafla iliyofanyika hivi karibuni katika ofisi za wizara jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Gray Mwakalukwa (kushoto) na Makamu wa Rais wa Mgodi wa African Barrick Gold (ABG), Deo Mwanyika (katikati) wakitia saini makubaliano ya kukabidhi Mgodi wa Tulawaka kwa STAMICO kutoka ABG, katika hafla iliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa ABG, Brad Gordon.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Gray Mwakalukwa (kushoto) akipeana mkono wa pongezi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mgodi wa African Barrick Gold (ABG), Brad Gordon (kulia) baada ya kukamilika kwa zoezi la utiaji saini makubaliano ya kukabidhi Mgodi wa Tulawaka kwa STAMICO kutoka ABG, katika hafla iliyofanyika hivi Dar es Salaam. Anayeshuhudia (katikati) ni Makamu wa Rais wa Mgodi wa ABG, Deo Mwanyika.

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesema kuanzia sasa serikali itakuwa na hisa katika migodi yote ya madini itakayoanzishwa hapa nchini ikiwa ni hatua ya kuhakikisha Watanzania wananufaika na rasilimali husika.

Profesa Muhongo aliyasema hayo hivi karibuni jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kutiliana saini makubaliano ya Serikali kutwaa umiliki wa Mgodi wa dhahabu wa Tulawaka kutoka kwa Kampuni ya African Barrick Gold (ABG).

Katika Makubaliano hayo, ambapo Serikali inawakilishwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), shirika hilo limeuchukua mgodi wa Tulawaka na baadhi ya leseni za utafutaji wa madini zinazozunguka eneo husika kwa gharama ya dola za Marekani milioni 4.5.

Aidha, kama sehemu ya makubaliano, STAMICO itachukua umiliki na usimamizi wa mfuko wa fedha za ukarabati wa mazingira, ikiwa kama sehemu ya mpango wa ufungaji wa mgodi huo na itachukua dhamana ya majukumu yaliyopita na ya baadae yanayohusiana na kufunga mgodi na ukarabati wa mazingira.

Waziri Muhongo, ambaye alishuhudia utiaji saini wa makubaliano hayo alisisitiza kuwa “lengo kuu la serikali ni kuhakikisha wananchi wananufaika ipasavyo na kufuta ile dhana iliyojengeka katika jamii kuwa watanzania hawanufaiki na rasilimali ya madini.”

Alifafanua kuwa STAMICO itamiliki na kuendesha mgodi huo kwa niaba ya watanzania na kwamba wataendeleza shughuli za uchimbaji na wakipata faida watauza hisa kwa wananchi wengi ili waweze kushiriki moja kwa moja katika umiliki.

Aidha, Profesa Muhongo alitumia fursa hiyo kusisitizia suala la wamiliki wa vitalu vya madini wasioviendeleza na kusema kuwa serikali imedhamiria kuwanyang’anya maeneo hayo na kuwapatia wachimbaji wadogo kama Rais Jakaya Kikwete alivyoagiza hivi karibuni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Kwakweli Tanzania tunachekesha Sana, barick walishatangaza kufunga mgodi wa tulawaka kwakuwa wameshamaliza dhahabu yote walioikusudia na baadhi ya wafanyakazi kuachishwa kazi
    Sasa Kama kampuni kibwa Kama barick tena yenye vifaa vya kisasa na tecknologia ya juu wamenyoosha mikono kuwa wamemaliza mzigo, stamico kweli wanataka kutuambia nini? Na je wamejipangaje kuhusu swala zima la mtaji? Acheni kutufunga kiini macho, kwakweli watanzania wengi watandanganywa Sana na Ni kwa sababu waziri anaongea technical Sana kiasi kwamba watanzania wengi hawamwelewi ila ajue si wote watakaodanganyika
    The geo

    ReplyDelete
  2. Bora tuendeshe wenyewe!

    Waweekzaji wamechimba weee miaka nenda miaka rudi leo wanfunga Mgodi eti Uzalishaji umeshuka na hauzai faida!.

    Je, Prof.Muhongo ile Kodi ya Uharibifu wa Mazingira uliyoanzisha kwa Migodi hao wamelipa? au ndio wanakabidhi mbuzi kwenye gunia?

    Pana umuhimu Makampuni ya Sekta Kuu zote Mfano

    1.Mawasiliano,
    2.Madini na
    3.Uzalishaji wa Viwanda,

    Yakaingizwa ktk MASOKO YA HISA NA YAKAMILIKIWA NA WANANCHI.

    NADHANI HAPATAKUWA NA MWEKEZAJI ATADAI ETI HAYALIPI!!!

    ReplyDelete
  3. Bado wale jamaa wa Tanzanite One Ltd. kule Mererani na wengineo zaidi pia nao wanyang'anywe!!!

    Ni wakati sasa wa kumpa Mtanzania Mzawa umiliki wa Madini na Rasilimali za nchi kama mnavyoona mchakato wa kuelekea Afrika ya Mashariki tayari wenzetu wameanza kumezea mate rasilimali zetu badala ya kusisitiza Muunganowenye tija!!!

    ReplyDelete
  4. Pia mweleze Mhe. Raisi aelekeze harakati hizo za uchukuaji umiliki kwenye Viwanda na Makampuni mengine pia zaidi ya Sekta ya Nishati na Madini!!!

    ReplyDelete
  5. Hebu tuelezeni kwani huo mradi si umeshafikia katika decommissioning phase?

    Yaani dhahabu yote imeshachimbwa tunakabidhiwa mashimo. Wanakimbia gharama za decommissioning hao.

    Ha ha haaaaa

    ReplyDelete
  6. mie nimefanya kazi Tulawaka hii ni sinema nyingine,sisi watanzania tunaakili kama sindano ya kushone,unaingiza uzi kwa nyuma halafu unashona kwa mbele,time will tell

    ReplyDelete
  7. no research no right to speak....walikochimba barrick si watakapochimba STAMICO ,,,ambako watachimba ni sehemu mpya kabisa ambayo haijawahi guswa na ipo nje ya mgodi ...tatizo ni sehemu ambayo itachimbwa may be kwa miaka miwili tu wakati target za BARRICK ni kuchimba sehemu ni za muda mrefu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...