Serikali wilayani Chato imeitaka Halmashauri ya Wilaya ya Chato kuendeleza mafunzo ya Mgambo kwa watumishi vijana ili waweze kujenga uzalendo na kuwa imara mahala pa kazi.

Wito huo umetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhe. Rodrick Mpogolo wakati akifunga mafunzo ya miezi mitatu ya Mgambo yaliyowashirikisha watumishi mbalimbali wa makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Chato yaliyofanyika kwenye uwanja wa Sekondari ya Chato.

Mkuu wa Wilaya amesema watumishi waliohitimu mafunzo ya Mgambo ni mfano mzuri wa kuigwa na watumishi wengine na hivyo kumwomba Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bw. Clement Berege kuhakikisha watumishi wote ambao hawakupitia jeshi la kujenga Taifa AU Mgambo kuhakikisha pia wanashiriki katika awamu nyingine ya mafunzo.

Katika risala yao kwa mgeni rasmi, wahitimu hao wameshukuru kwa kupata mafunzo hayo ambayo yamewajenga na kuwafanya wawe imara hata mahala pa kazi.

Mafunzo hayo yaliyoanza mwezi Julai 2013 yalifunguliwa na Mkuu wa Wilaya Mhe. Rodrick Mpogolo na ameyafunga leo ambapo jumla ya watumishi 65 wameitimu mafunzo hayo.
Watumishi Wanamgambo wakipita mbele ya Mgeni Rasmi.
Kamanda Mkuu wa kikosi cha kwanza Bi. Felicia ambaye ni katibu Muhitasi idara ya Afya akiongoza kikosi kupita mbele ya Mgeni Rasmi.
Wanamgambo baada ya kula kiapo.
Wahitimu ya Mafunzo ya Mgambo kwenye picha picha ya pamoja na mgeni rasmi pamoja na viongozi wengine wa Wilaya ya Chato.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...