Shirika la Maji Safi na Majitaka Dar-es-salaam (DAWASCO), linasikitika kuwatangazia wakazi wa jiji la Dar-es-salaam; Mji wa Bagamoyo kuwa Mtambo wa kuzalisha Maji wa Ruvu Chini utazimwa kwa wastani wa Saa 12 siku ya Jumamosi, Tarehe 09/11/2013 kuanzia saa 12 asubuhi hadi 12 jioni.
Mtambo wa Ruvu Chini utazimwa ili kuruhusu Mkandarasi kuendelea na upanuzi wa mtambo
Kuzimwa kwa mtambo wa Ruvu Chini kutasababisha maeneo yafuatayo kukosa Maji:
MJI WA BAGAMOYO VIJIJI VYA ZINGA, KEREGE NA MAPINGA, BUNJU, BOKO, TEGETA, KUNDUCHI, SALASALA, JANGWANI, MBEZI BEACH NA KAWE.
Maeneo Mengine ni : MLALAKUWA, MWENGE, MIKOCHENI, MSASANI, SINZA, KIJITONYAMA, KINONDONI, OYSTERBAY, MAGOMENI, UPANGA, KARIAKOO, CITY CENTRE, ILALA, UBUNGO MAZIWA, KIGOGO, MBURAHATI, HOSPITALI YA RUFAA MUHIMBILI, BUGURUNI, CHANGOMBE NA KEKO.
WANANCHI MNASHAURIWA KUHIFADHI MAJI NA KUYATUMIA KWA MATUMIZI YA LAZIMA.
DAWASCO INAWAOMBA RADHI KWA USUMBUFU UTAKAOJITOKEZA.
IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO
DAWASCO-MAKAO MAKUU
“DAWASCO TUTAKUFIKIA”



Hawa nao tumeshachoka izimeni tu moja kwa moja maana uwepo wenu hauonekani sie twanywa maji ya bonde hali ya kua mpo.
ReplyDeleteNinyi nanyi! Kwa mbwembwe tu ni kiboko. Nendeni basi mkafunge maji pale sayansi kijitonyama maana naona mafuriko yaliyopo tutasikia mengine.Pia msisahau pale maghorofani Mwenge hali bado ni tete.
ReplyDeleteTaarifa hii tungeipata walau wiki moja kabla na siyo siku moja kabla ya mitambo kuzimwa ingekuwa vema. Maana sidhani kama matengenezo hayo yalikuwa yakukurupuka
ReplyDelete