Jovin Shumbusho (pichani), aliyekuwa Principal Tax Investigations Oficer wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Idara ya Upelelezi wa Kodi, Amefariki dunia jana jioni katika hospitali ya Taifa Muhimbili kitengo cha "ICU". 

Jovin Shumbusho alisumbuliwa na uvimbe kwenye ubongo, uliopelekea aende nchini India kwa matibabu na kufanyiwa upasuaji. Alirudi Tanzania na kuendelea na dawa pamoja na uangalizi wa madaktari kwa muda wote.

Mipango ya mazishi tunasubiri taarifa rasmi kutoka kwa familia yake. Msiba upo nyumbani kwake Makongo Juu, Dar es Salaam. Tulimpenda sana Kaka yetu, Mshauri wetu, Kiongozi wetu, Mume kwa mkewe Eva, Baba kwa wanae Nancy na Jovin Junior, Mtoto kwa baba yake Mzee Shumbusho, lakini Mungu amempenda zaidi. Utukufu Juu kwa Mungu milele amina.

Bwana ametoa, Bwana ametwaa, Jina lake Lihimidiwe. Mungu Baba Mwenyezi aiweke roho ya Kaka Jovin Shumbusho mahala pema peponi. Amen.

Kwa niaba yangu binafsi na familia yangu na wana jamii wote wa blogu hii, tunatoa pole za dhati kwa familia ya Hayati Jovin Shumbusho na kuwaombea rehema za Mungu, uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu. Siku zote tunaamini Mungu ni mwema na tunashukuru kwa kila jambo. Sifa na Utukufu ni kwake Mungu Baba Mwenyezi. Amen.

Tutazidi kuwataarifu taratibu zote na mipango ya mazishi kadri tutakavyoipata.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Poleni sana familia, tumshukhuru Mwenyezi Mungu kwa yote.

    ReplyDelete
  2. R.I.P Jovin. Moderetor neno sahihi ni Marehemu siyo Hayati. Tunamuombea na familia yake ipate nguvu katika kipindi hiki kigumu. Amin

    ReplyDelete
  3. Kwa Mola tumetoka na kwake Mola sote tutarejea....poleni sana wana TRA na familia ya Shumbusho.
    Nawasihi sana muwe na moyo wa subira katika kipindi hiki cha mtihani.
    Mola atawapa subira na uvumilivu

    ReplyDelete
  4. Pole sana George na familia ya Mzee Shumbusho kwa msiba wa kaka yetu. Mungu ailaze roho ya Jovin mahali pema peponi, Amen.

    ReplyDelete
  5. Mwenyezi Mungu awape faraja wote walioguswa na msiba huu. Nikikumbuka miaka ile Shycom na baadae UD, jinsi alivyokuwa energetic...... ni vigumu kuamini hatunae tena. RIP Jovin

    ReplyDelete
  6. RIP kaka yangu Jovin...nilitegemea safari hii nikija bongo lazima nije kukuona baada ya kusikia habari za ugonjwa wako,lakini bahati mbaya mwenyezi mungu kakupenda zaidi...Amen.
    Mdau wa UK.

    ReplyDelete
  7. R.I.P
    TUTAKUKUMBUKA KWA MENGI MEMA UNCLE

    ReplyDelete
  8. Jovin Shumbusho was a true friend na ni watu wachache sana wenye moyo wa upendo kama yeye.Mwenyezi Mungu ampe nguvu mke wake na watoto pia

    R.I.P Brother

    ReplyDelete
  9. Poleni family ya Shumbusho, Mungu awe pamoja nanyi katika kipindi hiki kigumu.

    ReplyDelete
  10. R I P Jovin, I feel priviledged to have known you, I was very stunned to learn the sad news, still can’t believe that it really happened.
    My thought are with Eva, Nancy, Jovin Junior and the rest of the family, again R I P Brother!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...