MKOA wa Morogoro nao umeteuliwa kufanyika Tamasha la Krismas Desemba 26 mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ilieleza kuwa wametoa nafasi kwa Morogoro kutokana na kukidhi vigezo mbalimbali ambavyo kamati yake inavitumia.

“Tamasha la Krismas litafanyika Desemba 25 mwaka huu Uwanja wa Taifa Dar es Salaam na siku inayofuata itakuwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

“Tumeamua hivyo kutokana na sababu mbalimbali, lakini pia tumezingatia kuwapa nafasi wasanii wakimaliza tamasha la Dar es Salaam wapate muda wa kupumzika kisha wataondoka asubuhi taratibu kuelekea Morogoro, ambako hakuna umbali mrefu. Hivyo Morogoro wajipange kutupokea,” alisema Msama.

Tamasha la Krismas linaandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar es Salaam, ambayo pia huandaa Tamasha la Pasaka kila mwaka.

 Kwa mujibu wa Msama wanataka Tamasha la Krismas liwe bora zaidi kuliko la Pasaka kwa kualika wasanii maarufu kutoka nje na ndani ya Tanzania, ambapo tayari msanii  Upendo Nkone ameshathibitisha kushiriki tamasha hilo kubwa la nyimbo za kumsifu Mungu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...