Mheshimiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia mazingira akimkaribisha mgeni Rasmi kuongea na wajumbe katika ufunguzi wa semina ya wabunge na wawakilishi kuhusu maswala ya muungano Mjini Dodoma.
Mgeni Rasmi Mheshimiwa Mathias Chikawe akiongea na wajumbe wakati wa ufunguzi semina ya wawakilishi na wabunge kuhusu masuala ya muungano
Sehemu ya wajumbe wakifuatilia mada katika semina ya wawakilishi na wabunge kuhusu masuala ya muungano mjini Dodoma
Mmojawapo wa watoa mada Bwana Haule akiwasilisha mada katika semina hiyo mjini Dodoma.
Watanzania wameombwa kuwa wavumilivu na watulivu katika muda huu ambapo mchakato wa katiba unaendelea na kila mmoja ametakiwa kuweka mbele masahi ya taifa. Hayo yamesemwa mjini Dodoma na Waziri wa Sheria na katiba Mheshimiwa Mathias Chikawe ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa semina ya wabunge na wawakilishi kuhusu masuala ya muungano .
Aliongeza kuwa watu wote watambue kuwa katiba ni mali ya wananchi wote, ni dira ya wote na ni mwongozo muhimu kwa taifa ili kuhakikisha linasonga mbele na kwa kuzingatia misingi hiyo, ni wajibu wa kila mmoja kubaini kuwa hakuna aliye na haki zaidi ya mwingine katika mchakato huu. Katiba bora ni ileinayotokana na watu, inayoakisi matakwa ya watu na inayolenga kujenga na kustawisha maisha ya watu wan chi husika alisema.
Akimkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Muungano Mheshimiwa Samia Suluhu alisema Ofisi ya Makamu wa Rais imeandaa semina hiyo ili kutoa uelewa wa masuaa mbalimbali ya muungano. “Ofisi imeamua kufanya tathimini ya miaka hamsini ya utekelezaji wa masuala ya muunganona kuweka muelekeo mzuri wa kushughulikia masuala hayo” alisema .
Katika ufunguzi huo pia walikuwapo wataalamu mbalimbali ambao waliwasilisha mada zinazohusu muungano kwa wajumbe wote wa semina hiyo. Na pia wajumbe walipata nafasi ya kuuliza maswali na kuchangia.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...