
MkurugenziMtendaji wa
Kituo hicho, Bi. Juliet Kairuki alisema hayo wakati wa mkutano wa wadau
wa sekta hiyo kuwa wanahitajika kukitumia kituo chake ili waweze kupata
fursa zitakazo wawezesha kuwekeza zaidi katika uzalishaji zao la korosho.
“Kituo
chetu kinahamasisha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuwekeza katika
sekta hii ambayo ni muhimu sana katika uchumi wa nchi na ustawi wa
jamii,” Bi. Kairuki alisema na kuongeza kuwa kilimo cha korosho ni vyema kipatiwe msukumo zaidi. Alisema
kituo kimeweka vivutio mbalimbali kwa wawekezaji ambao wamejidhatiti
kuwekeza katika Kilimo, ikiwemo misamaha ya kodi kwa bidhaa za mitaji.
Aliongeza
Tanzania bado inahitaji wawekezaji kuwekeza katika Kilimo cha zao hilo,
viwanda vya kusindika na kuyatumia masoko ya ndani na nje ya nchi. Hali inaonyesha sekta hiyo haijafanya vya kutosha, hivyo amewaomba wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kukitumie kituo chake ili kufikia malengo ya serikali katika sekta hiyo.
Sambamba
na hilo alisema Tanzania inayomfumo mzuri wa sheria ambayo inavutia
kila anayetaka kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo ya Kilimo. Alisema
katika mazao ya kilimo, zao la korosho ni la tatu nchini katika
kuliingizia taifa mapato hivyo kunakila sababu ya wawekezaji kuingia
katika sekta hiyo ndogo.
Pia kuna taasisi za fedha za kutosha kwa ajili ya kupata huduma za kifedha kuendeleza miradi ya Kilimo.Aliongeza
kusema soko la hisa linaendelea kukua na imekuwa na msaada mkubwa
katika kuhakikisha shughuli za biashara zinazidi kuimarika.
Hata
hivyo aliwakumbusha wawekezaji wanaohitaji kuwekeza nchini kuhakikisha
wanatii sheria za nchi ili wasiweze kupata misukosuko inayotokana na
kuvunja sheria hizo. Mchumi
Mwandamizi Kitengo cha Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Bi.
Aneth Mathania aliwambia wawekezaji kuwa Tanzania ina ‘barcode’ yake
hivyo wakiwekeza mazao yao hayatapata shida ya soko.
“Tanzania
imeweka utaratibu mzuri kuhakikisha uzalishaji wa zao hilo katika
mnyoro wake wanapata faida, wakiwemo wakulima, wasindikaji na
wasafirishaji,”alisema. Pia
alisema vifungashia vya zao la korosho vinatolewa na Shirika la Viwanda
Vidogo (SIDO) hivyo fursa ya uzalishaji zao hilo ni kubwa.
Mkutano huo uliwaleta wawewkezaji wa ndani na nje wakiwemo ikiwemo sekta
binafsi, taasisi za kifedha, serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali
na wakulima wadogo kuzungumzia maendeleo ya sekta hiyo ya korosho.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...