Kaimu Mkurugenzi Mkuu toka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt. Hamza Kabelwa akionesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) cheti cha utambuzi walichopokea kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Mamlaka ya Usafiri Baharini(ZMA) kutokana na kuutambua mchango wao katika usafiri wa Baharini.Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari(MAELEZO) Bi. Georgina Misama.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu toka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt. Hamza
Kabelwa akionesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) ramani ya
Mwelekeo wa msimu wa mvua za
October hadi December 2013,ambapo rangi ya njano katika picha
inaashiria mvua za wastani na rangi ya kijani inaashiria mvua za chini
ya wastani. Kushoto ni Afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo Bi.Monica Shayo
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu toka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt. Hamza
Kabelwa akieleza kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) mikakati ya
Serikali katika kuendeleza huduma za hali ya hewa katika sekta ya
usafiri wa baharini,Visiwani Zanzibar na katika maziwa nchini,wakati wa
mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) leo Jijini
Dar es Salaam.Kushoto ni Afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo Bi.Monica
Shayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...