Mrembo wa Taifa Redds Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa yuko Kampala Uganda kwa mwaliko rasmi kutoka kampuni ya Arapapa Fashion House & Design ya nchini Uganda.
 
Redds Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa atakuwepo nchini Uganda kwa muda wa siku 5 hadi tarehe 9 Novemba 2013 anatarajiwa kurejea nchini.
 
Akiwa nchini Uganda ataungana na warembo wengine kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, Kenya, Rwanda, Burundi na wenyeji Uganda.
 
Pamoja na mambo mengine warembo hao watahusika pia katika kazi za jamii na baadaye kupanda jukwaani pamoja katika onyesho la mavazi lililoandaliwa na Kampuni hiyo.
 
Kampuni ya Arapapa imekuwa ikifuatilia kwa karibu mashindano ya urembo ya Miss Tanzania tangu mrembo Happiness  anyakue taji na waliazimia kumualika mrembo huyo kutembelea Uganda, jambo ambalo wamelitimiza.
 
Redds Miss Tanzania 2013 ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa  Shahada ya Juu katika Chuo cha Strathclyde  nchini Scotland, ameamua kuahirisha masomo yake kwa kipindi cha mwaka mmoja hadi hapo atakapovua taji mwishoni mwa mwaka 2014.
 
Mrembo Happiness Watimanywa atawakilisha Tanzania katika mashindano ya urembo ya dunia hapo mwakani.
 
HIDAN .O. RICCO.
PRO.
LINO INTERNATIONAL AGENCY LTD.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...