UPELELEZI wa kesi  ya wizi wa hati za kusafiria mali ya serikali, inayowakabili watu tisa akiwemo mwanamuziki Chingwele Che Mundugwao, umekamilika.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka, ametoa madai hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Sundi Fimbo anayesikiliza kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.

Kweka alidai kuwa kesi hiyo ilipangwa kutajwa jana lakini upande wa Jamhuri unatoa taarifa kwamba upelelezi wake umekamilika.
Aidha, alidai kuwa upande wa Jamhuri haujajiandaa kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali na aliomba mahakama kupanga tarehe ya kuwasomea.

Hata hivyo, hakimu alipiga kalenda kesi hiyo hadi Novemba 18, mwaka huu, itakapokuja mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa na washtakiwa wanaendel;ea kusota rumande.

Mbali na Che Mundugwao, washtakiwa wengine ni mwanafunzi  Ahsan Ali Iqbal au Ali Patel , raia wa Uingereza, ofisa  ugavi wa  Idara ya Uhamiaji, Shemweta Kiluwasha, Injinia Keneth Pius wa Kikosi  cha Zimamoto na Uokoaji, mfanyabiashara Ally Jabir, Rajab Momba, Haji Mshamu, Adam Athuman na Abdallah Salum.

Washitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka 11 ya kula njama za kutenda kosa, wizi wa hati 26 za kusafiria zenye thamani ya sh. milioni 1.3 mali ya serikali, kughushi hati za kusafiria, kukutwa wakimiliki hati zaidi ya moja halali.

Che Mundugwao na wenzake wanasota rumande kutokana na Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP), kuwasilisha hati ya kuzuia dhamana dhidi yao kwa maslahi ya taifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa



  1. Samahani sana Uncle na wadau naomba kuuliza inamaana kama namiliki passport ya Tanzania sirusiwi kumiliki passport ya nchi nyingine yeyeote ambayo nime ipata kihalali kabisaa???

    mfano nina passport ya Tanzania na tayari nakaribia kupata passport ya Singapore mbali na hyo nina passport ya ECOWAS issued by Federal Republic of Nigeria na passport zoote nimezipata kihalali kabisaa ikiwa ni pamoja na SPR- Sociol security number

    passport hizi zina saidia sana pale unapojua unasafiri nchi inayo hitaji VISA badala yake una switch to passport ambayo unaweza kuitumia as VISA free entry

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...