MSANII Upendo Nkone amekuwa wa kwanza kuthibitisha kushiriki
Tamasha la Krismas litakalofanyika Desemba 25 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex
Msama alisema jana kuwa tayari wamefikia makubaliano na msanii huyo na
kwamba bado wanaendelea na mazungumzo na wasanii wengine wa nje na
ndani
kuhakikisha tamasha hilo la nyimbo za kumsifu mungu linakuwa zuri.
“Nafurahi kuwajulisha wapenzi wa muziki wa kiroho kuwa
kamati yangu tayari imefikia makubaliano na Nkone, hivyo mambo yatakuwa mazuri
kadri siku zinavyokaribia,” alisema Msama.
Baadhi ya nyimbo za msanii huyo ni Upendo wa Yesu, Hapa
Nilipo, Mungu Baba, Yesu Aliniita, Sikiliza Nikuambie, Usiogope, Ijaposema,
Uumbaji, Yesu Nakupenda, Kanisa na Habari Njema.
Nyimbo nyingine ni Niacheni Niimbe, Nimebaki na Yesu,
Uniongoze Yesu, Nakuhitaji, Acha Uovu, Yesu Atakutunza na Moyo Wangu.Tamasha la Krismas linaandaliwa na Kampuni
ya Msama Promotion ya jijini Dar es Salaam, ambayo pia huandaa Tamasha la
Pasaka kila mwaka.
Kwa
mujibu wa Msama wanataka Tamasha la Krismas liwe bora zaidi kuliko la Pasaka
kwa kualika wasanii maarufu kutoka nje na ndani ya Tanzania na kwamba litakuwa
tamasha kubwa la nyimbo za kumsifu Mungu.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...