KAMPUNI ya Msama Promotions ambao ni waandaaji wa Tamasha la Krismas wametangaza viingilio vya tamasha hilo ambavyo kima cha chini ni shilingi 5000.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama viingilio vingine viti vya kawaida, 10000 VIP B na VIP A 20000.
Msama alisema watoto katika tamasha hilo watachangia shilingi 2000 ambako alitoa wito kwa jamii kujipanga kwa ajili ya tamasha hilo. Aidha Msama alisema viingilio katika mikoa yote litakakofanyika ni shilingi 5000 kwa wakubwa na watoto shilingi 2000na kuendelea kueleza kwamba wadau wajipange vilivyo kwa ajili ya tamasha hilo.
“Tunafanya taratibu za tiketi za tamasha hilo ambazo tumepanga zitoke Uingereza, ili kukwepa wizi utakaofanywa na baadhi ya wasiolitakia mema,” alisema Msama. Msama alisema wanajipanga vilivyo kuhakikisha wanakomesha ujanja unaotarajia kufanywa na wasiolitakia mema tamasha hilo ambalo dhamira yake ni kusaidia wanaoishi katika mazingirahatarishi wakiwemo yatima, wajane na walemavu.
Waimbaji katika tamasha hilo ni pamoja na Rose Muhando, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, John Lisu na New Life Band (Tanzania) na waimbaji kutoka nje ya Tanzania ni pamoja na Solly Mahlangu, Liliane Kabaganza, Solomon Mukubwa na Eiphraim Sekeleti.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...