Si jambo geni tena hivi sasa nchini Tanzania kusikia fulani kashambuliwa au kauawa kwa risasi.
Silaha za moto hapa nchini hasa zile zinazomilikiwa kiholela zimekuwa zikimilikiwa na kila anayetaka... kama vocha za simu. Hata mtu mwenye uwezo kidogo, na asiye na sababu ya kuwa na silaha anaweza kumiliki silaha nyumbani kwake. Bastola kwa sasa zimekuwa kama bidhaa ya utashi na watu wanazimiliki kama wanavyomiliki simu za mkononi.
Ungana
na Sophia Kessy (L) na Mubelwa Bandio (R) katika sehemu hii ya kwanza kuangalia
tatizo hili linaloonekana kuzidi kuathiri na kutishia maisha ya
waTanzania wengi.
Maajabu na Miujiza ya umilki wa Bastola Tanzania:
ReplyDeleteImekuwa ni Fasheni kwasasa unakuta mtu hata Mtaji wa LAKI TATU KWAKE MGOGORO, HUKU AKIWA NA UPUKU PUKU WA MADENI NA SHUGHULI ZAKE HAZIELEWEKI lakini Bastola kiunoni!!!
Hizi zama za Dijitali Watanzania wengi wetu zinatu changanya.
ReplyDeleteTunadhani maana yake ni Umiliki wa Silaha na hasa Bastola!
Utafiti ukifanyika inawezekana kabisa zaidi ya 75% wanaomiliki Bastola hawastahili kwa vigezo kuzimiliki!
ReplyDeleteTunaweza kushangaa kukuta Mmiliki wa Genge ama Chinga mwenye mauzo mazuri anapata sifa za kumiliki Bastola kwa kigezo cha Mapesa anayozungusha mkononi kuliko Mabosi wetu wa Kipedeshee ambao wengi wanaishi kwa Mabao, Vimeo na Madeni makubwa (KIMUONEKANO KWA NJE WAKIWA MABOSI NA KIHALISIA WAKIWA MAFUKARA)!
Naona tatizo sio umiliki. Tatizo ni anaye miliki amefanyiwa 'psychological evaluation'?
ReplyDeletekuna wengine wana matatizo ya akili(medically) lakini hajijui wala anayemlikisha silaha hajui namna ya ku-evaluate. Umiliki wa busara ni muhimu (azma za leo usalama ni hafifu; inabidi mtu ujilinde wewe na familia yako)
RIP Dr. Mvungi