Makamu wa Rais Dk Mohammed Gharib Bilal (katikati) akishirikiana na Naibu Waziri wa Fedha Janet Mbena kukambidhi kombe na cheti Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Rene Meza kufuatia Vodacom kushika nafasi ya tatu miongoni makampuni makuu yaliyolipa kodi kubwa mwaka 2013. Hafla ya utoaji tuzo kwa makampuni vinara ya ulipaji kodi imefanyika jijini Dar es salaam. Vodacom imeibuka pia kinara w aulipaji kodi katika sekta ya mawasiliano.
Naibu Waziri wa Fedha Janet Mbena (Kulia) akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Rene Meza tuzo ya ulipaji kodi bora ambayo Vodacom imeshinda katika sekta ya Mawasiliano iliyotolewa na Mamlaka ya Mapato Nchini – TRA katika hafla ya siku ya mlipa kodi iliyofanyika jijini Dar es salaam. Vodacom imeibuka pia ya tatu katika tuzo za jumla kitaifa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Rene Meza (kulia) na Meneja wa Mahusiano ya Nje wa Kampuni hiyo Salum Mwalim wakifurahia tuzo za ulipaji kodi bora ambazo Vodacom imeshinda mara baada ya kukabidhiwa wakati wa hafla ya siku ya mlipa kodi iliyoandaliwa na TRA. Vodacom imeshinda tuzo ya mlipa kodi mahiri katika sekta ya mawasiliano na mshindi wa tatu katika tuzo za jumla za ulipaji kodi kitaifa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Rene Meza akihojiwa na waandishi wa habari mara baada ya hafla ya siku ya mlipa kodi kitaifa iliyofanyika jijini Dar es salaam. Katika hafla hiyo Vodacom ilitangazwa mshindi wa kwanza kwa ulipaji kodi katika sekta ya mawasiliano na ya tatu kitaifa miongoni mwa makapuni yote ya baishara hapa nchini yaliyolipa kodi.






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...