Mkurugenzi wa Kampuni Frontline,Hellen Kiwia (kulia) akizungumza na Waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika mapema leo,wakati akitoa tathmini ya Safari ya Baadhi ya Waandishi wa Habari pamoja na Mbunifu wa Mavazi,Sheria Ngowi ya kwenda Nchini Afrika Kusini kwa mualiko maalum kutoka Bodi ya Utalii ya nchi hiyo,ambapo walihudhulia Maonyesho ya Mavazi ya Mercedes Fashion Week 2013 yaliyofanyika Jijini Pretoria pamoja Utalii wa Maeneo mbali mbali nchini humo.Wengine pichani ni baadhi ya Wandishi waliokuwepo kwenye safari hiyo pamoja wadau.
Mwanalibeneke Othman Michuzi akizungumza machache kuhusiana na safari hiyo wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari uliofanyika leo kwenye Duka la Mavazi la Sheria Ngowi,lililopo Mtaa wa Bizwagi,Masaki jijini Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja ya Wadau walikwenda nchini Afrika Kusini hivi karibuni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...