DSC_0394
Mama Tunu Pinda akikaribishwa kufunga maonyesho ya wiki ya Wakinamama Wajasiriamali na Mratibu wa Kitaifa wa Programu ya kuendeleza wajasirimali wanawake Tanzania kutoka ILO, Noreen Toroka. kushoto kwa Mama Pinda ni Mwenyekiti wa MOWE, Bi Elihaika Mrema na
DSC_0354
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akifunga rasmi Maonyesho ya Wanawake Wajasirimali (MOWE) katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, maonyesho hayo ya wanawake wajasiriamali yalikuwa ya wiki nzima ambapo wakinamama wanapata nafasi ya kuonyesha na kuuza bidhaa mbalimbali Usindikaji, Mvinyo, Batiki kwa wakazi wa jijini.
DSC_0337
Mratibu wa Kitaifa wa Programu ya kuendeleza Ujasiriamali kwa wanawake Tanzania toka Shirika la Kazi Duniani (ILO) Noreen Toroka akizungumza wakati hafla ya kufunga maonyesho hayo ambapo amesema wiki nzima ilikuwa ni maonyesho wanawake toka sehemu mbalimbali nchini Bara na Visiwani wamepata wasaa wakubadilishana mawazo na mbinu za Kibiashara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Ndio ni kweli....inabidi tufundishwe hivi kuanzia udogoni. Unajua waswahili wanasema, "Samaki mkunje angali mbichi" ehhhhh

    ReplyDelete
  2. Tatizo bidhaa zinaonekana katika maonesho na yakiisha basi.

    Mara nyingi nashauri taasisi husika angalieni uwezekano katika kila Mkoa kuwe na eneo maalum la bidhaa za Tanzania mnaweza ita eneo"made in Tanzania area" ama lolote mtakalobuni lenye kuleta maana kama hiyo.

    Ni ushauri tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...