JUMLA ya watoto 137 na wajawazito 19 hufariki dunia kila siku nchini Tanzania kwa matatizo yanayotokana na uzazi. Vifo vya watoto pekee wanaopoteza maisha kutokana na matatizo hayo kwa mwaka hufikia 50,000 kwa nchi nzima.
Takwimu hizi za kusikitisha zimetolewa leo jijini Dar es Salaam na Meneja Mradi wa mpango wa 'Wajibika Mama Aishi', Bw. David Lyamuya toka Taasisi ya Utepe Mweupe katika semina ya wahariri na waandishi wa habari waandamizi.
Lyamuya alisema mbali na idadi hiyo kubwa ya akinamama pamoja na watoto kupoteza maisha yapo matukio mengine ya vifo ambayo hayaingizwi kwenye takwimu, hali inayoonesha huenda vifo hivyo ni zaidi ya takwimu halisi zilizopo.
Alisema kuna kila sababu kwa mamlaka husika kwa kushirikiana na jamii kulivalia njuga suala hilo ili kuhakikisha vifo vya mama na mtoto vinakoma. Aidha alisema licha ya uhimizaji wa wajawazito kuhudhuria klini bado idadi kubwa hasa vijijini wanajifungulia nyumbani kutokana na umbali mrefu wa sehemu zinapotolewa huduma za afya.
"...Sisi tumefanya utafiti katika Mkoa wa Rukwa kuangalia hali ya upatikanaji huduma za afya kwa wajawazito. Yapo maeneo mama aliyefikia hatua ya kujifungua (mwenye uchungu) hutakiwa atembee kilomita 94.5 ndiyo anakutana na kituo cha afya, sasa mtu aliye na hali kama hiyo hawezi kutembea umbali mkubwa kiasi hicho hivyo hulazimika kujifungua nyumbani," alisema Lyamuya.
Aidha aliongeza kuwa taasisi ya Utepe Mweupe (The White Ribbon Alliance) kwa sasa inaendesha kampeni ya miaka mitatu ya "Wajibika Mama Aishi" ikiwa ni moja ya hatua ya kushawishi kila mmoja kuwajibika kuhakikisha anakabiliana na vifo vya akinamama na watoto vinavyotokea hasa wakati wa kujifungua.
Hata hivyo aliwataka wanahabari kuhakikisha wanatumia nafasi zao kutoa mchango wa kuvishavishi vyombo husika na wanajamii kwa ujumla kupambana na vifo vya akinamama na mtoto.
Meneja Mradi wa 'Wajibika Mama Aishi', David Lyamuya akiwasilisha mada katika semina ya wahariri na waandishi wa habari iliyofanyika Regency Hotel jijini Dar es Salaam.
Rais wa UTPC, Kenny Simbaya akiwasilisha mada kwenye semina hiyo
Baadhi ya wahariri na waandishi wa habari waandamizi wakihudhuria semina hiyo
Mheshiwa Lowasa anafaa,akifuatiwa na Mh.Wilbroad Slaa.
ReplyDeleteMh.Lowasa angeendelea kuwa waziri mkuu mpaka mwisho naamini kuna watu wangepelekeshwa mzobemzobe nginja nginja mpaka wangekoma.
Watanzania tumezoea kwenda too slagish kama konokono.
Maendeleo ni kufanya kazi kwa bidii kwa mbio bila kuchoka.
Kwa mwendo huu nadhani hatutafika mapema jamani.
Kuhusu Chama gani kinafaa,jamani mimi sijaona kama chama cha CCM kama kimepoteza umaarufu kiasi cha kunyimwa ridhaa ya kuongoza Tanzania.Bado kwa maoni yangu kinafaa, japo chama cha Chadema nacho kina mazuri yake.
TATIZO TANZANIA SI VYAMA,BALI NI WATU WENYEWE WANA MATATIZO.
UTAFITI UFANYIKE KUHUSU MAMBO YANAYOKWAMISHA TANZANIA ISIPATE MAENDELEO YA HARAKA KATIKA NYANJA ZOTE.NAAMINI CCM AU CHADEMA SI TATIZO.
2015 tunataka raisi atakaye Kuwa na mikakati madhubuti ya kuboresha sekta ya afya. Kabla hatuja mpigia kura aainishe bayana mikakati aliyo nayo ya kuboresha sekta ya afya. Tukijiridhisha Kuwa mikakati yake ni madhubuti na inatekelezeka ndio tutampigia kura.
ReplyDelete