Na Hassan Abbas

Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM) umemuomboleza Rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela kwa kumtaja kuwa ni kiongozi wa mfano. Mandela (95) alifariki usiku wa Alhamisi iliyopita baada ya kupambana na maradhi na umri mkubwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa juzi na makao makuu ya APRM yaliyoko mjini Midrand, Afrika Kusini, kifo cha Mandela ingawa kimeliachia Bara la Afrika huzuni kuu lakini Mzee Mandela anapaswa kushukuriwa kwa mambo makubwa aliyoyafanya kwa ajili ya binadamu.

“APRM ingependa kuwasilisha salamu zake za rambirambi kwa watu wa Afrika Kusini, familia, marafiki, wenzetu wengine katika Bara la Afrika na dunia kwa ujumla, kufuatia kifo cha Nelson Rholihlahla Mandela, Rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika Kusini,” ilisema taarifa hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...