Namuonea huruma huyo kocha mpya wa Manchester United. Leo najidai kuwa Sheikh Yahya mpya, natabiri jamaa atapigwa teke karibuni. Recodi yake yatisha. 

Man U wamefungwa na Everton timu ambayo haijaifunga Manu tangu 1992, na Moyes alipokuwa kocha wa Everton hakuwahi kuifunga Man U..Juzi Manu tena wamefungwa na Newcastle timu ambayo haijaifunga Man U tangu 1972. Na vipigo vyote vimetokea nyumbani kwenye uwanja wao. Audhubillah 

Mdau Ibrahim

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Wadau wa soka wanaamini kuwa ManU walikuwa wakibebwa wakati wa enzi za Sir Alex Ferguson.

    ReplyDelete
  2. Mdau, kocha hapaswi kulaumiwa hata kidogo kwa timu kufanya vibaya, kumbuka amechukua mikoba timu ikiwa na wachezaji karibia wote ni walemavu kwa maana wamekamuliwa kwa zaidi ya miaka mitano mfululizo na serious SAF. kwa hiyo hata ukiangalia kwa makini utagundua ile kasi ya mchezaji mmoja mmoja imepungua sana. Apewe fursa aunde kikosi kingine na mambo yatanyooka, kumbuka hata SAF alitaka kufukuzwa mwanzoni.

    ReplyDelete
  3. Kuna Mkenya kajiuwa baada ya matokeo ya Jumamosi.
    http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2520757/Kenyan-football-fan-commits-suicide-Manchester-United-lose-Newcastle-United-Old-Trafford.html

    ReplyDelete
  4. kila lenye mwanzo huwa na mwisho , na aliye juu msubiri chini, na aliye chini msubiri juu , ukitafakari maneno haya utaelewa maisha na mizunguko yake , hakuna cha milele ktk maisha ya kibinadamu , lazima ukubali kuna kushinda na kushindwa falsafa hii huwa inakubalika katika michezo , lakini wanasiasa ni wagumu kuelewa wanataka kila siku iwe chama fulani tu kinatawala hata wakishindwa basi hughushi kura mradi washinde , ni vyema kwa wanasiasa wakachukua mifano hii inayotokea ktk michezo na kuiga uzalendo wa wanamichezo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...