Mhe. Liberata Mulamula,Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico amekutana na Mhe. Dk. Juma Akil, Katibu Mkuu,Wizara ya Mawasilano na Miundo Mbinu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar aliyefika Ubalozini Tanzania House,Washington DC,Marekani. Balozi Mulamula alimshukuru Katibu Mkuu huyo kwa kupata wasaa wa kumtembelea Ubalozini hapo ambapo pia alimshukuru kwa kuhudhuria sherehe za miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika Washington DC mwishoni mwa wiki iliyopita.
Pichani Mhe.Balozi Liberata Mulamula akiwa katika picha ya ukumbusho na Mhe.Dk.Juma Akil,Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasilano na Miundo Mbinu wa Serikali ya Mpinduzi ya Zanzibar.
Mhe.Dk. Juma Akil, Katibu Mkuu,Wizara ya Mawasiliano na Miundo Mbinu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar(katikati) akiwa na mkewe Bibi Fatma Akil (kulia) na Bw. Suleiman Saleh,(kushoto) Afisa wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika picha ya ukumbusho katika kuadhimisha sherehe za uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika Washington DC mwishoni mwa wiki iliyopita.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...