Wananchi wakijaribu kufukua udongo ili kuopoa  miili ya watu walofukiwa na kifusi katika machimbo ya Moramu eneo la Pumwani wilaya ya Moshi vijijini huku wananchi wengine wakishuhudia
 Uongozi wa mkoa wa Kilimanjaro ukiongozwa na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama ukishuhudia zoezi la ukoaji wa miili ya watu hao.
 Juhudi za kuokoa waliofukiwa zikiendelea
 Gari aina ya fuso lenye namba za usajili T 167 AQG ambalo marehemu wa tukio hilo walikuwa wakijaza Moramu likiwa limeangukiwa na ngema iliyokatika na kusababisha vifo vya watu sita. Kwa picha zaidi zilizopigwa na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii  mkoa wa Kilimanjaro BOFYA HAPA


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Kuhusu maelezo ya picha ya mwanzo, neno 'kuopoa' lina tofauti kubwa mno na neno 'kuokoa' ambalo ndilo ingefaa utumie.

    ReplyDelete
  2. poleni wafiwa. terrible to die that way! Dear lord may rest their souls in peace Amen.

    ReplyDelete
  3. Hii ni habari ya kusikitisha sana. Poleni woote mlioguswa na tukio hilo. Nimesikitika zaid pale nilipokuwa nasikiliza radio moja hapa moshi ikitoa taarifa hiyo kwa njia ya kejeli flani km Eti ile nyumba unayojenga ilipata moram kutoka machimbo hayo!!? Hii ni kejeli mbovu kwa chombo cha habari! Je mamlaka zinazosimamia vyombo hivi wanatuambiaje sisi ama wenye radio hizo wasiwasi?
    Si hapa tuu Radio hizi zimekuwa zikitangaza mambo yasiyo staha mara kadhaa bila kuonywa .... hayumkini watangazaji hawa hawana taaluma ya kutosha. Naomba wasidiwe jamani.

    ReplyDelete
  4. Ivi hawa huwa wanatembelewa kweli na wataalum husika ktk kuangalia usalama na mazingira yao ya kazi?......au ndio aaah watajua wenyewe!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...