Watanzania waishio Korea Kusini walipata bahati ya kutembelewa na Mh. Bernard Membe; Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa siku ya tarehe 8 Disemba 2013, katika Chuo Kikuu cha Dongguk jijini Seoul.
Katika mkutano huo, Waziri alifurahishwa sana na
muamko, uelewa, na malengo kabambe ya Jumuiya ya Watanzania nchini Korea (TANROK) katika kujiendeleza na kuendeleza nchi yao.
Waziri
alitoa taarifa ya hali ya uchumi, siasa, na kijamii nchini Tanzania na kuahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wanadiaspora ili waweze kutumia
vizuri elimu na ujuzi wanaopata ughaibuni katika kuendeleza nchi yao.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe akisaini
kitabu cha Wageni alipotembelea Jumuiya ya Watanzania waishio nchini Korea
Kusini jijini Seoul.
Mh. Bernard Membe (wapili toka kushoto)
akijibu hoja mbalimbali za Watanzania
waishio Korea Kusini. Katikati ni
Mwenyekiti wa TANROK Bw. Rayton
Kwembe, akifuatiwa na Mkurugenzi wa
Idara ya Asia na Australia Balozi Mbelwa
Kairuki, na wa mwisho kulia ni Katibu wa
TANROK Bw. Innocent Lugendo. Wa
kwanza kushoto ni afisa wa Ubalozi wa
Tanzania nchini Japan anayeshughulikia
Masuala ya Korea Kusini, Bw. Francis
Mossongo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe na Mkewe wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi wa idara ya
Asia na Australia katika Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Mbelwa Kairuki wakipozi kwa picha ya pamoja na baadhi
Watanzania Waishio nchini Korea Kusini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...