Na Abdulaziz Lindi
Katika heka heka za kuaga mwaka 2013 usiku wa kuamkia leo mji wa Lindi
ulitikisika baada ya mashabiki kujitokeza kushuhudia onyesho la
Msanii nyota wa Muziki wa kizazi kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
alipokuwa akitoa burudan kabambe katika Tamasha la kudumisha Amani na
Maendeleo lililodhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Mtama,Mhe Bernard
Membe na kufanyika katika Uwanja wa Ilulu Manispaa ya Lindi na kutoa
burudani ya nguvu ambayo ilizikonga nyoyo za mashabiki waliodhuria
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’akiwapagawisha mashabikiw wake walikuwa wamefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Ilulu,Mkoani Lindi.
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’sambamba na madansa wake,wakitoa burudani ya nguvu kwa mashabiki wao.
Mbunge wa Jimbo la Mtama ambae pia ni Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Bernard Membe akipokea salamu toka
kwa Diamond alipokuwa akitoa salam za mwaka mpya kwa wana Lindi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...