Mwanamuziki mahiri toka nchini Uganda Dr. Jose Chameleone akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza kuhusiana na Tamasha lililopewa jina la 'Badilisha Concert' litakalofayika leo 24 dec 2013 katika uwanja wa CCM Kirumba kuanzia saa 12 jioni hadi majogoo kama sehemu ya kuikaribisha sikukuu ya Christmass. Pembeni yake anaonekana meneja wake na mwisho kabisa kulia ni mmoja wa wadhamini wa Tamasha hilo Mr. James Njuu wa K Vant Gin.
Mwanamuziki mahiri toka nchini Uganda Dr. Jose Chameleone akisalimiana na mmoja kati ya wasanii wa Jambo Squard mbele kidogo ni Dogo Dee na mwisho kabisa (kushoto) katika mstari ni mwanamuziki Bob Haisa ambao wamefika kumpa sapoti katika show ya Badilisha Concert itakayofanyika leo CCM Kirumba Mwanza. 
Kwa mujibu wa mratibu wa tamasha hilo Denis (kushoto) kutoka Silver Intertainment amesema kuwa kampuni yake imeamua kuweka kiwango kidogo cha kiingilio ili watu wote wa Kanda ya Ziwa waipate zawadi ya mwaka kushuhudia burudani kali.
"Zawadi nyingi huwekwa kwenye boxi lakini hii yaani mimi ni zawadi iliyo nje ya boxi maalum kwa wakazi wa Mwanza" pia Jose Chameleone anasema kuwa najivunia kuwa Mwanza mji ambao kwangu ni sawa na nyumbani.
Jose Chameleone amekwepa kulizungumzia suala lake la hivi majuzi kukumbatiana na mdogo wake Weasal na binamu yake Radio ile hali walikuwa kwenye bifu kali akisema yote yatafanyika lakini undugu utabaki pale pale akisita kuendelea kulizungumzia suala hilo kwa undani akisema hawezi kuzungumzia masuala ya familia nje ya familia anaheshimu utamaduni wa kiafrika.
Jose akiwa na wanahabari wa Mwanza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. The mdudu,hivi hiyo show FID Q na wanamuziki kibao toka hapo Mwanza wasingeiweza,watu wa Mwanza kumbe mkotofauti sn na sisi wana Morogoro huku moro hatumpi mtu chance ya kuzarau wanamuziki wetu Afande Sele Oyeee moro kwanza Uganda baadae

    ReplyDelete
  2. KAMA KILA MTU NI DAKTARI BASI MIMI SISOMI TEMA KWASABABU ELIMU HAINA MAANA TENA, KAMA UNAWEZA TU KUITWA DAKTARI HATA BILA KUSOMA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...