Mwanamzuki mwimbaji  wa Kimataifa wa nyimbo za Kiroho a.k.a Injili kutoka nchini Afrika Kusini,Solly Mahlangu pichani kati akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwal J.K.Nyere jijini Dar jioni ya leo.Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa tamasha la krisimasi,Bwa.Alex Msama na wadau wengine waliofika kumlaki mwanamuziki huyo mahiri anaetarajiwa kutumbuiza hapo kesho kwenye uwanja wa Taifa wakati wa tamasha la krisimasi.
 Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotions Ltd,inayoandaa tamasha la Krisimasi,Bwa.Alex Msama akizungumza na baadhi ya Wanahabari kuhusiana na ujio wa mwanamuziki wa Afrika Kusini,Solly Mahlangu aliyewasili jioni ya leo jijini Dar tayari kuungana na wanamuziki wengine wa nyimbo ya Injili kwa ajili ya kutumbuiza hapo kesho kwenye tamasha la Krisimasi,ambalo linasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wake.
Mwanamuziki wa nyimbo za Injili,Solly Mahlangu akiwapungia mikono mashabiki wake waliofika kumlaki mara baada ya kuwasili jioni ya leo kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwal J.K.Nyere jijini Dar jioni .Kulia kwake ni Mwenyekiti wa tamasha la krisimasi,Bwa.Alex Msama na wadau wengine waliofika kumlaki mwanamuziki huyo mahiri anaetarajiwa kutumbuiza hapo kesho kwenye uwanja wa Taifa wakati wa tamasha la krisimasi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hivi vitambaa vya bendera ni vya nini Bongo? Kwani kuna baridi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...