Action Music Tanzania (AMTZ) inatangaza fursa kwa watu wote kujiunga na mafunzo ya kupiga ala za muziki yanayoanza desemba 19 mwaka huu, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wanamuziki wa kupiga ala na kufanya maonesho kwa weledi na utaalamu zaidi.
Mafunzo yanayotolewa ni pamoja na upigaji wa ala za muziki zikiwemo gita, kinanda, tarumbeta, saxophone, konga, drum set, na upigaji wa ngoma za asili. Pia yatatolewa mafunzo ya ‘body percussion’ yaani matumizi ya mwili katika kutengeneza midundo ya muziki.
Mafunzo hayo yanafanyika kwenye ofisi za AMTZ zilizopo maeneo ya Mwenge karibu na magorofa ya jeshi ambapo ili kujiunga na mafunzo haya wasiliana nao kwa simu namba 0686928828 au barua pepe, actionmusictz@yahoo.com, Like Facebook Page au tembelea www.amtz.org
 Mwalimu Abeid Mussa akitoa maelekezo ya wakati wa mazoezi ya kufanya onyesho la muziki
 Mwalimu wa Kinanda Prosper Shirima (katikati) akifundisha
Mwalimu wa Gita, Ashimba (kushoto) akitoa maelekezo ya namna ya kupiga chombo hicho

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...