Katibu wa chama cha CHADEMA wilaya ya Chunya,Bwa Bryson Mwasimba akionesha kadi yake ya chama hicho akiirejesha kwa chama cha CCM,mara baada ya kuachia ngazi,kwenye mkutano wa hadhara uliofanywa na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana,uliofanyika kwenye kata ya Lupa Tinga Tinga,Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.Ndugu Kinana na ujumbe wake yuko mkoani Mbeya kwenye ziara kukagua utekelezaji wa Ilani ya chama,kukagua miradi mbalimbali ya chama na wananchi sambamba na kusikiliza matatizo ya wananchi na namna ya kuyatafutia ufumbuzi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akimkabidhi kadi ya chama cha CCM,Katibu wa chama cha CHADEMA Wilayani Chunya,Bwa.Bryson Mwasimba aliyeamua kujiuzuru wadhifa wake mapema leo na kurejea CCM,huku umati mkubwa wa watu uliofika kwenye mkutano wa hadhara ukishangilia kwa mayowe na miluzi,uliofanywa na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana,uliofanyika kwenye kata ya Lupa Tinga Tinga,Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.
 Bwa.Bryson Mwasimba akionesha kadi ya CCM mara baada ya kutangaza kuachia ngazi CHADEMA.
 Bwa.Bryson Mwasimba akizungumza mbele ya wananchi na wanachama wa CCM kuhusiana na kuachia ngazi kwake na kurejea chama cha CCM mapema leo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Siku katibu wa ccm akihamia CHADEMA upost pia, usiwe na biasness!

    ReplyDelete
  2. Wewe hapo juu achana na ankali wetu, kila chama kikimletea vitu anarusha (angalia hapo juu), inaonesha ni jinsi gani nyie CDM mlivyo na mioyo ya shari na ukorofi. Hahahahaaaaa mmeshashitukiwa, msimmalizie hasira zeni ankali hapa. Malizeni yanayowasibu ndio muanze vya kuanza. Bundi mnalo hilo hadi 2015 hahahaaaa poleni mwe!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...