Hospitali ya Wilaya ya Pangani ni moja ya Vituo vya kutolea huduma za matibabu ambazo zilitembelewa na Waandaaji wa vipindi vya elimu kwa umma.
 Mganga Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Dk. Dennis Ngaromba akitoa maelezo mafupi kuhusu mradi unaoendeshwa na NHIF wilayani humo.
 Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya waandaji wa vipindi vya elimu kwa umma wakimwangalia motto aliyezaliwa hospitalini hapo na mmoja wa wanufaika wa mradi wa NHIF.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa katika wodi ya akina mama ambao ni wanufaika wa mradi huo.
Washiriki wakivuka kwenye kivuko kuelekea Kituo cha Afya cha Mwera ambacho ni miongoni mwa vituo vinavyotoa huduma kupitia mradi huo.

Na Mwandishi Wetu, Pangani

MRADI wa kusaidia akina mama wajawazito wasio kuwa na uwezo unaoendeshwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kushirikiana na Benki ya watu wa Ujerumani (KfW) katika mikoa ya Tanga na Mbeya umesaidia kuongeza mwamko wa akina mama kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Mwamko huo umetokana na elimu kubwa inayoendelea kutolewa  na NHIF kwa walengwa, lakini pia huduma zinazotolewa kwa akina mama hao baada ya kuandikishwa katika vituo vinavyoendesha  mradi huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...