Na Mwandishi Wetu

Wafalme wa muziki wa dansi nchini bendi pizani za Msondo Ngoma “Baba ya Nuziki’ na Mlimani Park Orchestra (Wana Sikinde Ngoma ya Ukae)  watapambana siku ya Krismasi katika viwanja vya TCC Club Chang’ombe.

Mpambano huo umeandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts na kudhaminiwa na Konyagi na Nipashe.
Mratibu wa mchuano huo Joseph Kapinga amesema pambano hilo litakuwa la kusherekea sikukuu ya Krismasi na kufunga mwaka 2013.
Kapinga alisema kuwa pia pambano hilo litaamua ni bendi gani bora ya mwaka huu.


Mratibu huyo alisema kila bendi itapiga kwenye jukwaa lake ili kuondoa malamiko ya kuhujumiwa. Kila bendi itapiga muziki jukwaani kwa muda wa saa moja kabla ya nyingine kupanda.


“Litakuwa ni pambano la aina yake ukizingatia kila bendi ina vyombo vipya walivyopewa na kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (Konyagi). Pia tutakuwa na michezo aina mbalimbali ya watoto,” alisema Kapinga.

Alisema mchuano huo utaanza saa nane mchana hadi majogoo.
Wadhamini wengine wa shindano hilo ni pamoja na gazeti la Nipashe, Saluti5 na CXC Africa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. MTOTO (Sikinde) ANAIMBA:
    ..................................
    Eeee mama, eeee mama, eeee mama nipeleke kwa baba

    Hata nikila makande kwa kachumbari bora nikiwa kwa baba yengu X 3.

    Kwa kosa hili ulilonitendea mbele za Mungu huna Sheria!

    ,,,,REAPAT CHORRUS ABOVE.


    Siku hiyo ndio tutafahamu Mtoto (Sikinde) anayeimba hapo juu Baba yake ni nani!

    ReplyDelete
  2. 1.Hiba. 2.Kipenzi Edita. 3.Barua toka kwa mama 4.Clara. 5. Hapendeki .6. Shemeji Issa. 7. Konjesta. 8. Gama. Kassim no.1. 9. Ni nani aliyemdanganya mchumba wangu .10.Kiu yajibu. 11.Naomi. 12. Nalala kwa taabu. 13.Kupenda sio ndoto .14. Bubu 15.Uzuri wa mtu sio sura .16. Naheshimu ndoa............Hivi ndio vibao vitakavyoiangamiza msondo ngoma siku hiyo.....hhahaahhaahahaahhaha

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...