Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikagua Mradi wa ujenzi maji safi wa Izumbwe ,Iwindi unaojumuisha vijiji nane ambavyo ni Shongo,Igale,Horongo,Itimu,Mwampalala,Izunbwe,Iwindi na Mwashiwala,Mradi huo umejengwa katika kijiji hicho kufuati vijiji hivyo kukosa maji safi kwa muda mrefu.Mradi huo unatekelezwa chini ya programu ya Taifa ya usambazaji wa maji safi vijijini na usafi wa binafsi na mazingira na ulianza rasmi septemba 2013 na ulitarajiwa kukamilika mnamo Mei,2014.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na baadhi ya wanachama wa CCM,wakishiriki
ujenzi wa Zahanati katika kijiji cha Shamwengo,Kata ya Inyala Wilaya ya
Mbeya Vijijini Mkoani Mbeya mapema leo.
Katibu
wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt.Asharose Migiroakishiriki
ujenzi wa Zahanati katika kijiji cha Shamwengo,Kata ya Inyala Wilaya ya
Mbeya Vijijini Mkoani Mbeya mapema leo.
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya,Mh Abbas Kandoro sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya
mjini,Mh.Norman Sigala pichani shoto wakishiriki ujenzi wa Zahanati
katika kijiji cha Shamwengo,Kata ya Inyala Wilaya ya Mbeya Vijijini
Mkoani Mbeya
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Mh Abbas Kandoro na
Wajumbe wengine wakitoka kushiriki na kukagua mradi wa ujenzi wa
zahanati ya Shamwengo,Kata ya Inyala Wilaya ya Mbeya Vijijini Mkoani
Mbeya
Pichani ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Ujumbe wake wakifanya mkutano na Wajumbe Halmashauri kuu ya CCM wilaya katika ukumbi wa Chuo cha Ufundi Mbalizi,wilaya ya Mbeya Vijijini mkoani Mbeya.
Michigan...Amerika inafurahi sana!!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteMbalizi hapo hakuna maji kabisa lakini vyanzo vya maji vipo hasa chemichemi za mto fwizimu. Kinana na timu yako + Dr Norman tunnaomba mlishughulikie hilo before 2015. Huyo mbunge wa sasa ni mzigo kwa wapiga kura wake
ReplyDelete