Klabu ya riadha ya Hameenlinnan Tarmo  ya Finland imeeleza kuguswa na changamoto wanazopata wanariadha wa Tanzania na kujitolea kuwasaidia pea 20 za viatu 'spikes' kwa ajili ya maandalizi ya michezo ya Jumuiya ya Madola.

Hata hivyo Chama cha Riadha Tanzania (RT) kimeeleza kuwa licha ya sapoti hiyo bado wakimbiaji wao wanachangamoto nyingi kipindi hiki wanachojiandaa kuweka kambi tayari kwa michezo ya madola.

"Wanariadha wanaoingia kambini ni 35 ambao wanahitaji vifaa, chakula, na mahitaji muhimu, klabu ya Hameenlinnan Tarmo imefungua njia tunaomba na wadau wengine watuunge mkono," alisema Naibu rais wa RT, William Kallaghe.

Kigogo huyo wa RT alibainisha kuwa wanariadha hao wanahitaji maandalizi thabiti ili kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye michezo ya madola na kuongeza kuwa sapoti ya Watanzania ndiyo itakayowaongoza kufanya vizuri kwenye michezo hiyo.

Akikabidhi msaada huo mwakilishi wa klabu ya Hameenlinnan Tarmo, Ari Koivu alisema huo ni mwanzo wa kuisaidia riadha ya Tanzania na kuongeza kuwa watakuwa bega kwa bega na RT kuhakikisha wanafanya vizuri kimataifa.

RT imewaita wanariadha 35 ambao iliwateua kwenye mashindano ya Umisseta, taifa na wale wenye rekodi nzuri kwenye mashindano ya kimataifa kuanza kuunda kikosi cha taifa kitakachoweka kambi mapema Januari kujiandaa na michezo ya madola.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...