Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akiwasalimia wananchi alipokua akiwasili uwanja wa Uhuru wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru leo jijini Dar es salaam.Kushoto ni Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akipokea salam ya Rais na kupigiwa mizinga 21 kutoka kwa gwaride la vikosi vya majeshi ya Ulinzi ya Tanzania leo uwanja wa Uhuru mara baada ya kuwasili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akikagua gwaride la vikosi vya majeshi ya Ulinzi na usalama leo uwanja wa Uhuru wakati wa maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Kaka Michuzi tuweke sawa hapa.Nilivyosoma historia ya Tanzania kuitwa hivyo ni kwamba:
    tarehe 9 Desemba 1961 ambayo sasa tunatimiza miaka 52,Tanganyika ilipata uhuru kutoka kwa wakoloni ambao ni Uingereza.Zanzibar ilipata 1963 na mwaka 1964 Tanganyika na Zanzibar zikaungana kuunda TANZANIA sasa unavyosema miaka 52 ya uhuru wa Tanzania huoni kama tunapotosha historia yetu.

    ReplyDelete
  2. huwezi kusema uhuru wa Tanzania uncle, hizi ni Sherehe za uhuru wa Tanganyika.....

    ReplyDelete
  3. Acheni chokochoko. Hampendi mabadiliko! Kwanini mnaendelea kulazimisha majina ambayo kimsingi yamebadilika? Mbona wengi wakisoma wanaendelea kuitwa kwa title mpya Professa...Dr. Mhe...Askofu... Shekhe....acheni ushabiki wa siasa usioleta mandeleo. Tumieni vichwa vinu kufikiria mambo ya maendeleo.

    ReplyDelete
  4. Hhahahahahahaha...hahahahha. Uncle kakabwa koo na wadau hapo juu.....kwa muda wa miaka 51 wenda maswali dizaini hii hayakuwepo...wengi wetu tulijionea sawa tu...hasa baada ya kuburudika na gwaride la maafande kisha kujirudia nyumbani huku tukiadithiana jinsi maafande walivyokua mahili...lakini leo tunauliza je kuna usahihi ktk tarehe......hahahahha ni maswali mazuri ila sitarajii majibu toka kwa Uncle....tehetehetehetehe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...