Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Ankal, huna "hard copy" ya hiyo speech ya JK utuwekee hapo pia? wengine tuko nje ya mji kwahiyo network inasua-sua kweli hivyo hatuwezi kabisa kuunganisha sentensi za anchozungumza JK hapo .....Tafadhali!

    ReplyDelete
  2. Hongera
    That was a beautifully crafted and masterly delivered speech.When people started to get too sad, he threw a pebble into the pond that caused a ripple of laughter by questioning as to whether or not Mbeki had returned his Tanzanian travel documents.Then the end was the icing on the cake
    Hongera muheshimiwa.

    ReplyDelete
  3. Hotuba safi.ni ile ile aliyoitoa tarehe 09-December-2013 siku ya sherehe za uhuru(Miaka 52 ya Uhuru).
    Humu kwenye blog yetu huwa kuna ubishi wa Lugha gani itumike kufundisha kwenye shule zetu kati ya Kiingereza na Kiswahili.Sasa maeneo kama haya tusidanganyane, Kiingereza kinakuwa na nguvu sana na Mwingereza ataendelea kutawala dunia au mnasaemaje wadau jamani?.PERIOD

    David V

    ReplyDelete
  4. excellent speech JK , nafikiri tuwe wenye kufikiri , kutumia lugha ya kiswahili kufundisha mashuleni , huwa inaturudisha nyuma wakati mwengine na tunashindwa kwenda na wakati , vitabu vingi na majarida mengi ya kisayansi na utafiti huandikwa kwa kiingireza , mikutano yote ya kitafiti huzungumzwa kwa kiingerea.

    ReplyDelete
  5. Mdau wa tatu kuhusu lugha itumike kufundishia mashuleni. Nadhani ni kiingereza tu na kweli mwingireza ataendelea kututawala si utani. Ila lugha hii unaeleweka kila kona ya dunia uendako. Naunga mkono kiingereza na inaleta raha sana ukikijua asikudanganye mtu. Wenzetu nchi nyingi za ulaya ambazo watoto wao wanajifunza lugha hii ya kiingereza mashuleni ikifika umri fulani watoto wao wanakwenda uingereza kufanya kazi kwa muda au hata kusoma ila kuwa na confidence kuitumia lugha hii ya kiingereza.

    ReplyDelete
  6. Congratulation Mr. President

    ReplyDelete
  7. Baada ya Hotuba ya Raisi Kikwete,

    Wadau ktk Hoja la Lugha kwenye Elimu tuzingatie ya kuwa MTAALA PIA NI MUHIMU na pia isijengeke mtazamo potofu wa kuamini kuwa KUELEWA SANA KIINGEREZA NDIO KUELIMIKA!

    ReplyDelete
  8. Hotuba Kali sana!

    Pana Mdau mmoja mwenzangu (Sesophy) mara nyingi huwa ananishangaa nikimwita Mhe. BALOZI DAKITARI Raisi Jakaya Kikwete!

    Je, Kwa matendo yake mengi JK, utendaji wake JK, Kwa uzito wa maneno hayo na mengi anayo yatoa bado haistahili tumwite hivyo?

    ReplyDelete
  9. Sisi wengi tuna issue na lugha ya kiingereza, kwani jamaa walikuwa our masters for a long time na walituibia sana. Lakini
    lugha yao sasa ni lugha ya dunia,there are more English speaking people in the world than raia wa uingereza.I have seen East European IT students here working as waiters etc during college terms to learn the language. Lugha ni tamu sana hasa kama unaijua vizuri na kwa undani na uwe na ile sprachgefuhl.
    ibrahim

    ReplyDelete
  10. Speech nzuri sana, nakubaliana na madau hapo juu pia Kiingereza kitumike kufundishia level zote za elimu yetu-Lugha si element ya utumwa kivile, na hata kama kwani hatukutawaliwa?

    ReplyDelete
  11. Wadau "Watumwa mamboleo" hapo juu. Habari ilikuwa ni uzuri, umhimu na kiwango cha juu cha hotuba ya Mhe. Rais wetu, lakini ninyi wenye kukumbatia utamaduni wa kizungu na msivyojipenda wenyewe, habari ya hapa ikawa ni gumzo la lugha. Wazungu wangapi wanaishi Tanzania lakini karibu wote hawakithani kiswahili badala yake wanatukuza lugha zao kwa vile ninyi wenyewe mnaidharau lugha yenu. Hakuna atakaye kuheshimu iwapo wewe mwenyewe hujiheshimu na kujithamini. Habari ndiyo hiyo kwa leo ninyi nyote hapo juu mnaoshabikia kiingereza. Mhe. Rais katoa hotuba nzuri yenye kiwango cha juu sio kwa sababu alitumia kiingereza ndipo ikaonekana hotuba yake nzuri hivyo. Angaweza hata kutumia kihoxa ama kizulu bado ingebaki hivyo. Mnatu aibisha sana huko mliko.
    - Mhoja - Sweden

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...