Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyesha Kitabu cha Mpango Mkakati wa Haki za Watoto 2013-2017, wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Sita ya Kitaifa ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani na Maadili, uliofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (katikati) akikata utepe kuashiria kuzindua Kitabu cha Mpangokazi wa Taifa wa haki za Binadamu wa mwaka 2013-2017, wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Sita ya Kitaifa ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani na Maadili, uliofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo. Wa pili (kushoto) ni Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe na Naibu wake, Angela Kairuki (kushoto) Mwenyekiti wa Tume ya Hakiza Binadamu na Utawala Bora, (wa pili kulia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya Sita ya Kitaifa ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani na Maadili, katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe, akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi, Makamu wa Rais Dkt. Bilal, kuhutubia na kufungua rasmi, maadhimisho hayo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mashiriki, Taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za Kiserikali, wakimsikiliza Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alipokuwa akihutubia wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Sita ya Kitaifa ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani na Maadili, uliofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...