TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Malkia wa Uholanzi Mhe. Maxima anatarajiwa kuwasili nchini tarehe 11 Desemba, 2013 kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
Mhe. Maxima ambaye pia ni Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Mfumo Jumuishi wa Fedha katika Maendeleo atapokelewa na mwenyeji wake, Mke wa Rais, Mhe. Mama Salma Kikwete kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Baada ya kuwasili, Mhe. Maxima atafanya mazungumzo rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Ikulu, Dar es Salaam pamoja na kushiriki katika Dhifa ya Kitaifa.
Aidha, tarehe 12 Desemba 2013, Malkia Maxima atafanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhe. Mhandisi Christopher Chiza, Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Saada M. Salim na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Benno Ndulu.
Siku hiyo hiyo Mhe. Maxima atazindua rasmi Mfumo Jumuishi wa Fedha wa Taifa katika hafla itakayofanyika Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Mfumo huo unalenga kuwanufaisha Wanawake na Vijana, hususan katika kuchangia usalama wa chakula, kilimo na maendeleo Vijijini.
Mhe. Maxima ataondoka Dar es Salaam tarehe 13 Desemba, 2013 kuelekea Dodoma ambako ataendelea na ziara yake kwa kutembelea mashamba ya zabibu katika Kijiji cha Gawaye pamoja na kuzungumza na Wakulima. Mashamba hayo yanasimamiwa kwa ushirikiano kati ya Shirika la Chakula Duniani (WFP), Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD).
Mhe. Maxima anatarajiwa kuondoka nchini siku hiyo hiyo jioni kurejea Uholanzi.
IMETOLEWA NA:
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA,
DAR ES SALAAM.
10 DESEMBA, 2013
Ankali, sahihisho kuhusu taarifa ya Malkia Maxima.
ReplyDeleteNchi ya the Netherlands mfalme wake ni King Willem-Alexander na mkewe ambaye ni mzaliwa wa Argentina anaitwa kwa jina rasmi la Princess Maxima na siyo Malkia Maxima a.k.a Queen Maxima.
Mfalme Willem-Alexander alitawazwa kuwa Mfalme wa the Netherlands baada ya mama yake ambaye alikuwa ndiye Malkia wa The Netherlands, Queen Beatrix 'kungatuka'tarehe 30, April 2013.
Ndiyo maana Princess Maxima anatapokelewa rasmi na Mke wa mh. Rais Kikwete, Mama Salma kama mwenyeji wake.
Wellcome. KARIBU TANZANIA
ReplyDeleteThe Queen of Netherland.
Mdau wa kwanza unayeomba sahihisho: Ankali hajakosea kabisa kumuita mgeni wetu Queen au Malkia. Alikuwa akiitwa princess kipindi kile yule mheshimiwa ambaye sasa ni mfalme kule Udachini alipokuwa akinyemelea taji hilo. Sasa basi, kwa kuwa ameolewa katika ufalme, na mumewe ndio sterling kule...inabidi aitwe QUEEN CONSORT. Kwa hiyo atabakia kuitwa Malkia. Ila kama ingekuwa kinyume chake, yaani mtawala wa kiti angekuwa mwanamke kama Bibi wa UK, mumewe hatoweza kuitwa King...atabakia kuwa Prince. Na kama bado kuna tatizo kidogo, jaribu kupitia family trees za tawala mbalimbali za kifalme. AHSANTE
ReplyDeleteMsaada katika tuta.
ReplyDeleteJamani nachanganyikiwa na michango ya wadau hapo juu, kwa nini mume wa wa Queen (Queen aliye head of state) hawezi kuitwa King( lakini mke wa King (ambaye ni head of state)anaweza kuitwa Queen?
Je huu ni mtizamo wetu maana Mke wa Rais haitwi Rais-Mama ktk mfumo wa republic a.k.a jamhuri
Wakazi wa Uholanzi tunaomba ufafanuzi kuhusu suala hili la kiitifaki.
Mdau
Globu ya Jamii
Mdau #2 ametowa ufafanuzi sahihi kama nchi ina mfalme wa kiume kama Holland,Spain,Sweden na Norway mke ataitwa Queen.Kama nchi ina mfalme wa kike kama England,Denmark mume ataitwa Prince. Ankal yupo sawa.
ReplyDeleteMikidadi-Denmark