Mkurugenzi wa shule ya kimataifa ya Southern Highlands Mafinga Bi Mary Mungai akimkabidhi cheti mmoja kati ya wahitimu wa mahafali ya 13 shule hapo ,kulia kwake ni kaimu meneja wa Benk ya wananchi Mufindi (Mucoba) Bw Ben Mahenge
Walimu na wafanyakazi wa shule ya Southern Highlands Mafinga wakiwa katika picha ya pamoja na mkurugenzi mtendaji wa shule hiyo Bi Mary Mungai kushoto wa kwanza .
.............................. .............................. ....
Na Francis Godwin
MAENDELEO mazuri ya ufaulu wa wanafunzi wa shule ya kimataifa ya Southern Highlands Mafinga mkoani Iringa iliyoisukuma benk ya wananchi Mufindi (MUCOBA) kujitokeza kuunga mkono jitihada za elimu katika shule hiyo .
Shule ya Southern Highlands Mafinga imeonekana kuivutia zaidi benki hiyo ya MUCOBA kutokana na rekodi yake nzuri ya kufaulisha vizuri wanafunzi wote darasa la saba tangu ilipoanzishwa mwaka 1997.
Kiwango cha elimu kinachotolewa katika shule ya kimataifa ya Southern Highlands Mafinga kinaisukuma benk ya wananchi wilaya ya Mufindi (MUCOBA) kuahidi kutoa kiasi cha Tsh milioni 2.5 kwa ajili ya kuwafungulia akaunti katika benk hiyo wanafunzi waliofanya vema matokeo ya mtihani huo mwaka huu.
Bw Ben Mahenge anasema kuwa moja kati ya sababu iliyopelekea benk yake kujitokeza kuunga mkono jitihada za shule hiyo ni kutokana na ufaulu mzuri wa mitihani ya Taifa ya darasa la saba ambayo shule hiyo imeendelea kuongoza na hivyo kutoa heshima kwa wilaya ya Mufindi na Tanzania kwa ujumla .
Kwani anasema kuwa mbali ya benk hiyo kuendelea kutoa mikopo mbali mbali ila imekuwa karibu zaidi na shule hiyo ya Southern Highlands Mafinga ambapo mkurugenzi wake Bi Mary A. Mungai ni mmoja kati ya wateja wakubwa wa benk hiyo kutokana na
wazazi wote wanaosomesha watoto katika shule hiyo kulipia ada kupitia benk hiyo hivyo kiasi hicho cha fedha kilichotolewa na MUCOBA ni kutambua mchango wa shule hiyo katika uendelezaji wa benk hiyo.
" Kati ya wateja wakubwa wa benk ya MUCOBA ni pamoja na shule ya Southern Highlands Mafinga na wazazi ambao wanasomesha watoto hapo kutokana na wazazi wa watoto wanaosomesha hapo hulipa ada kupitia benk yetu .....hivyo kwa ajili ya kumpongeza mkurugenzi wa shule hiyo kwa kuzidi kuiunga mkono benk yetu bado tunazidi kuwahamasisha wananchi wa wilaya ya Mufindi na nje ya mkoa wa Iringa kujiunga nasi"
Mahenge anasema kuwa benk hiyo imeendelea kutoa mikopo mbali mbali kwa wateja wake ikiwemo mikopo ya ujenzi wa nyumba bora , ujasiliamali na mikopo ya kuendeshea biashara .
Hata hivyo Mahenge anasema kuwa wanafunzi watakaonufaika na msaada huo ni yule aliyefanya vizuri katika matokeo ya mtihami wa Taifa wa darasa la saba pamoja na mwanafunzi Aida Mhagama ambae aliibuka mshindi wa jumla katika masomo mbali mbali na kupongezwa wakati wa mahafali ya darasa la saba ya shule hiyo .
Anasema fedha hizo zitaingizwa katika akaunti zao baada ya kufunguliwa na benk hiyo kwa lengo la kusaidia kuwasomesha elimu ya sekondari pindi watakaojiunga na elimu hiyo ya sekondari mapema mwakani .
Mkurugenzi mtendaji wa shule hiyo Bi Mary Mungai ambae amepata kuwa afisa elimu shule za msingi anasema kuwa shule imekuwa ikifundisha kwa kiingereze, yaani english medium school, imefaulisha tena mwaka huu 2013 wahitimu wote wa darasa la saba na kuiwezesha kuwa katika asilimia mbili (2%) ya juu ya shule zote zenye kufaulisha vizuri kitaifa, na katika 10 bora kati ya shule 449 za mkoani Iringa.
“…Tunawapa hongera wahitimu hao na kuwatakia maendeleo mazuri kokote waendako. ….pia tunawapongeza wazazi/walezi, tunawatakia kila la heri kuwaendeleza watoto wao kufuatia msingi huu ulio bora waliopata kutoka Southern Highlands School.”
Anasema pia uongozi wa shule hiyo hautaacha kuwapongeza walimu, kwa kazi kubwa wanayoendelea kuifanya kila siku kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu iliyo ya kiwango cha juu.
“ Sisi tunapokea watoto kutoka pande zote za nchi na watakaotaka watoto wao wajiunge na Southern Highlands School, nafasi zipo kwa wanafunzi wa chekechea, darasa la 1, 2, 3, na 5 kwa wanafunzi wote na darasa la 4 na la 6 kwa wanaotoka shule za english medium.”
Anasema kuwa toka shule hi yo ilipoanzishwa mwaka 1994 kama Day Care na Pre-school na mwaka 1997 kuanza shule ya msingi imekuwa ikifanya vizuri na hakuna mtoto aliyepata kufeli .
“Shule yetu mwaka 2001 shule ilitoa wanafunzi wa kwanza wa darasa la Saba na wanafunzi walikuwa 17, wote walifaulu vizuri na wote walichaguliwa kuendelea na masomo ya kidato cha kwanza”
Anasema katika matokeo ya mitihani ya darasa la 7 ya mwaka 2001 Southern Highlands School ilishika nafasi ya kwanza kitaifa katika mitihani ya Somo la Kiingereza.
“ Tulimshukuru Mungu na tunaendelea kumshukuru Yeye kwa kuwezesha watoto wetu wa Southern Highlands School, kufaulu vizuri, kwa kishindo” alisema Bi Mungai
Hata hivyo anasema kila mwaka wanafunzi wote wamekuwa wakifaulu mitihani ya kitaifa ya darasa la saba na wote kuchaguliwa na kuendelea na masomo ya Sekondari.
“Mwaka huu tena wanafunzi wote wa darasa la saba 47 waliomaliza mwaka huu 2013, wamefaulu na kuchaguliwa kuendelea na sekondari”
Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Bw Omary Mahinya anasema kuwa katika moja ya vielelezo kuwa shule hiyo ni bora nchini ni wazazi kutoka mikoa karibu yote ya Tanzania kupeleka watoto wao hapo .


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...