Mwaka mpya unakuja,tuufanyeje?
Mabaya yaliyopita,tuyazikeje?
Neema Tuliyopata,tuienzije?
Neema tukiipata,tufurahije?
Huzuni ikitufika,tuishikeje?

Na mdau Hija Saleh,
Holland.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. SALAM ZA MWAKA MPYA (MAONI)

    Kwanza mshukuru Mungu, hilo ndio moja namba,
    Sitengane kwa mafungu, umoja wetu hayumba,
    Kwa matamu na machungu, ni MOLA zidi muomba,
    Kila kheri ndugu zangu, mpya mwaka unakuja.

    Mabaya yaliyopita, si kamili walimwengu,
    Sana twabakia juta, omba 'tughufiri' Mungu,
    Tena sirejee hata, natowa nasaha zangu,
    Jema baya kitupata. sheria zina vifungu.

    Tuloipata neema, isitugawe mafungu,
    Wachoyo siwe daima, sing'ang'ane hiki changu,
    Towa moyo si lazima, 'jaza' yetu ikwamungu,
    Si petu hapa tahama, tunapita ndugu zangu.

    Tufurahie neema, ziwe tamu au chungu,
    Tushukuru kila jema, japo kiwa duchu fungu,
    Hadhari zetu 'kalima', sifike kufuru Mungu,
    Sisonone kikunyima, pengine si lako fungu

    Ikitufika huzuni, ni 'Qadari' yake Mungu,
    Siwe mikono shavuni, na kulia kwa machungu,
    Huyu yule halaani, kimbizana kwa marungu,
    Tupima zetu imani, hilo kaahidi tangu.

    Nawatakia kila la kheri kwa ujao MWAKA MPYA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...