Meya wa London,Haruna Mbeyu akimpongeza Wakili Saidi Yakubu mara baada ya sherehe za kuwaapisha.Wengine pichani ni wana diaspora waliojitokeza kumpongeza kwa kuapishwa kuwa wakili.
Mdau wa Watanzania waishio nchini Uingereza,Bi Mariam Mungula akielezea tuzo ya "Award of Recognition" waliyompa Wakili Saidi Yakubu ambae amekuwa ni miongoni mwa wadau wanaosukuma gurudumu la maendeleo ya Diaspora.Tuzo hiyo inayosomeka "Award of Recognition,Presented to Mr Saidi Othman Yakubu,Advocate and Private Secretary to the Deputy Speaker,Parliament of Tanzania for his Outstanding Contribution and Being a Role Model to Tanzanians in Diaspora" imetolewa na taasisi ya East Africa Education Foundation - UK kwa Wakili Yakubu kwa mchango wake kwa wana diaspora.
Wakili Saidi Yakubu baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo katika picha ya pamoja na wana diaspora waliomkabidhi.Wa pili kulia ni mai waifu wake,Bi Dida.
Picha ya pamoja na mawakili wapya walioapishwa siku hiyo na Jaji Mkuu,Jaji Kiongozi na viongozi wengine wa tasnia ya sheria nchini.
Mdau Yakubu akiwa na familia yake baada ya kulamba nondoz ya uwakili siku hiyo. Picha kwa Hisani ya East Africa Education Trust- UK.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. haya chapeni kazi watanzania wanahitaji kuhudumiwa kwa huduma bora kushinda zile zilizoko nchi zingine zinazoitwa zimeendelea

    ReplyDelete
  2. Hongera saana wakili-Mkuu Yakubu
    kweli kabisa juhudi zako ni mfano mkubwa wa kuigwa. Mafanikio yako ni faida kubwa kwetu na zaidi kwa vijana wa Tanzania.Mchapa kazi wa kiwango cha uhakika nilishughudia nilipokuwa mgeni wa mwaliko bungeni
    Mikidadi-Denmark

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...