Ujumbe kutoka Tanzania ulioshiriki kwenye
Mkutano wa Mawaziri wa Shirika la Biashara la Dunia (WTO) uliofanyika mjini
Bali, Indonesia kuanzia tarehe 3 – 6 Desemba, 2013 ukiongozwa na Mhe. Dkt
Abdallah O. Kigoda (Mb), Waziri wa Viwanda na Biashara.
Mheshimiwa Dkt. Abdallah O. Kigoda (Mb.), Waziri wa Viwanda na Biashara akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Biashara wa Misri Mhe Mounir ABDEL NOUR na ujumbe wake walipokutana katika Mkutano wa Shirika la Biashara la Dunia (WTO) uliofanyika mjini Bali, Indonesia hivi karibuni.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Abdallah O. Kigoda (Mb) akijadiliana jambo na Ndg. Lucas Saronga, Mkurugenzi wa Idara ya Utangamano wa Biashara Wizara ya Viwanda na Biashara kwenye Mkutano wa Mawaziri wa Shirika la Biashara la Dunia uliofanyika mjini Bali, Indonesia kuanzia tarehe 3 – 6 Desemba, 2013
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Abdallah O. Kigoda (Mb) akijadiliana jambo na Waziri wa Biashara na Uwekezaji wa Finland Mhe Alexander STUBB kwenye Mkutano wa Mawaziri wa Shirika la Biashara la Dunia uliofanyika mjini Bali, Indonesia kuanzia tarehe 3 – 6 Desemba, 2013. Mwingine ni Ndg. Lucas Saronga, Mkurugenzi wa Idara ya Utangamano wa Biashara Wizara ya Viwanda na Biashara Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...