Mkuu wa Huduma za Rejereja za Kibenki wa Benki ya NBC Tanzania, Mussa Jallo (wa pili kushoto) akizungumza katika  hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa droo ya kwanza ya promosheni ya ‘Weka Upewe’ ya benki hiyo ambayo washindi wanne walikabidhiwa pikipiki mpya aina ya Honda. Hafla hiyo ilifanyika pamoja na uchezeshwaji wa droo ya pili katika Tawi la NBC Ubungo jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza na Wateja Wakubwa, Andrew Massawe, Meneja katika kitengo hicho, Dorothea Mabonye na Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Chiku Saleh. 
 Mmoja wa washindi wa droo ya kwanza ya promosheni ya NBC Weka Upewe, Festo Mukerebe (kulia) akionyesha ufunguo wa pikipiki aina ya Honda, mara baada ya kukabidhiwa na Meneja Kanda wa NBC, Rachel Mwalukasa (kushoto) katika hafla hiyo iliyofanyika katika Tawi la Ubungo jijini Dar es Salaam leo.
 Mkuu wa Huduma za Rejereja za Kibenki wa Benki ya NBC Tanzania, Mussa Jallo (kulia) akikabidhi zawadi ya pikipiki mpya aina ya Honda kwa Dk. Isaya Mpelumbe aliyopokea kwa niaba ya mtoto wake, Edna Ndumbaro aliyeshinda katika droo ya kwanza ya promosheni hiyo.
 Meneja wa NBC Tawi la Ubungo, David Nsimba (kushoto) akikabidhi funguo ya pikipiki mpya aina ya Honda kwa Hassan Khamis aliyepokea kwa niaba ya Prof. Peter Maina wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambaye naye aliibuka kidedea katika droo ya kwanza ya promosheni ya NBC Weka Upewe.
Mmoja wa washindi wa promosheni ya Weka Upewe ya benki ya NBC, Festo Mukerebe akitoa shukrani zake kwa benki ya NBC mara baada ya kukabidhiwa zawadi yake ya pikipiki mpya aina ya Honda. Kushoto ni Meneja Masoko wa NBC, Alina Maria Kimaryo na kushoto kwa Alina ni mke wa Festo, Alphoncena Mukerebe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...