Ofisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya
Wilaya ya Nkasi, Oscar Mdenye
Na TheHabari.com

JESHI la Polisi Wilaya ya Nkasi kupitia dawati la Jinsia na Watoto, linamshikilia Pius Jacob Mkazi wa Kijiji cha Chala kwa kosa la kuoa mtu na dada yake, ambapo mdogo mtu alikuwa ni mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Kabwe wilayani Nkasi.

Jacob alikamatwa na Polisi wa Dawati la Jinsia na watoto Kituo cha Nkasi ikiwa ni wiki moja tangu amchukue kwa nguvu binti huyo wa darasa la tano (umri miaka 12) na kuja kuishi naye kama mke na mume huku akiwa tayari amemuoa binti mwingine wa kwanza mwenye umri wa miaka 16 ambaye pia ni dada wa binti wa pili.

Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Dawati la Jinsia Nkasi, CPL-Anna Kisimba alisema walimfuatilia Jacob na kumkamata baada ya wao kupewa taarifa na mmoja wa majirani wa mtuhumiwa kuwa alikuwa akiishi kinyumba na wanafunzi hao.

“…Tulikuwa katika ziara zetu za kawaida zilizoambatana na siku 16 za kupinga ukatili tukizunguka baadhi ya vijiji vya wilaya yetu, ndipo raia wema walituarifu kuwepo kwa tukio hilo na kuanza kufuatilia hatimaye kumkamata mtuhumiwa,” alisema Kisimba.

Tayari mtuhumiwa huyo amefikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Desenba 10, 2013 kwa kosa la kumuoa mwanafunzi na kubaka katika Mahakama ya Wilaya ya Nkasi, Mkoa wa Rukwa kujibu mashtaka ya tuhuma zake.

Akizungumzia tukio hilo, Ofisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri wa Wilaya ya Nkasi, Oscar Mdenye alisema baada ya kufuatilia zaidi wamebaini hata binti (16) aliyemuoa wa kwanza alikuwa ni mwanafunzi haijulikani alitumia mbinu gani za kumpata na kuanza kuishi naye kama mke na mume.
Mkuu wa Dawati la Jinsia Nkasi, CPL-Anna Kisimba (kushoto) akipitia kitabu cha orodha ya matukio ya dawati hilo. Kulia ni msaidizi wake.

Aidha ameongeza kuwa kwa mujibu wa tarifa ambazo walizipata kutoka kwa majirani inadaiwa binti wa pili alimpata kwa kutumia nguvu na vitisho, kwani alimfuata nyumbani kwao na kudai anakuja kuwasalimia lakini baada ya kufika kwake alimjulisha binti huyo kuanzia sasa wewe ni mke wangu na kuanza kuishi naye.

“…Hadi Polisi na Ofisi ya Ustawi wa Jamii tunafikiwa na taarifa hizo inadaiwa mtuhumiwa huyu alikuwa tayari ameishi na binti huyu wa pili kwa wiki nzima nyumbani kwake, na majirani walijua baada ya binti wa pili (12) kuanza kulalamika kwao kuwa alikuwa amechukuliwa kwa nguvu na kulazimishwa kuolewa,” alisema Mdenye.

Juhudi za kumpata mtuhumiwa kuzungumzia tuhuma zake hazikuweza kuzaa matunda baada ya kuwa mahabusu akisubiri mwenendo wa kesi yake inayomkabili.

Hata hivyo matukio ya ukatili yanayoripotiwa polisi kupitia Dawati la Jinsia na Watoto Wilaya ya Nkasi yamekuwa yakipungua kutoka mwaka hadi mwaka, kwani kwa mujibu wa takwimu za dawati hilo kwa mwaka 2012 kulikuwa na kesi 224 za ukatili zilizoripotiwa, ilhali kwa mwaka 2013 jumla ya kesi 143 zimeripotiwa wilayani hapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Pius Jacob, umeonyesha UBASHA WA FUNGA MWAKA!

    HIYO YA KWAKO NDIO KWA HERI 2013!!!

    Yaani unaoa wanawake wawili ndugu?

    Tena zaidi ya hapo wapo chini ya miaka 18?

    Huku ukiwa u-Mkristo na kuwa dini yako hairuhusu kuwa na mke zaidi ya mmoja!

    Ungekuwa wewe ni mtu wa Pwani tungesema ohhh ndivyo watu wa Pwani walivyo !,sasa bahati nzuri wewe na hao wasichana ni watu wa bara!

    ReplyDelete
  2. we anon wa kwanza acha udini. Kwani kuitwa Pius maanake mkristo? jina halina dini, ni lebo wazazi wake walimpa kwa sababu alikuwa hajijui.

    ReplyDelete
  3. matatizo ya bure. ungekuwa mpenzi wao bila kuoa palikuwa hamna kokoro.

    ReplyDelete
  4. Wewe mdau wa kwanza SHIKA ADABU YAKO. ACHA UFARA. Inakuwaje unatudhalilisha sisi watu wa PWANI????

    ReplyDelete
  5. Duuu kweli watu wengine wachafu sana jamani!

    Hivi wewe mtu unakuta wasichana wawili ndugu moja wa familia moja!

    Unaowa wote wawili!, unawachanganya Kitandani!,

    Bila haya wala aibu unamshushia zipu na kumlalia kitandani mkubwa na siku inayofuata unamshushia zipu na kumlalia kitandani mdogo wake!

    Hapo Ustaarabu upo wapi?

    ReplyDelete
  6. Mdau wa 4 usilalamike na kudharau watu wenigine bila kutafakari!

    Watu wa Pwani miaka nenda miaka rudi wamekuwa wakifedheheshwa sana na kusemwa kwa tabia kama aliyoionyesha Pius Jacob mkazi wa Bara.

    Zama nyingi zilizopita Dunia ilikuwa inafikiri ya kuwa Ufirauni kama Ulawiti ni mambo ya nchi za Kiarabu!, sasa Dunia inashuhudia Ulawiti ukishamiri Nchi za Magharibi na hasa Ulaya na Marekani hadi kufikia Ndoa za Jinsia moja na kudai Haki kwenye Mabunge na Seriklini!!!

    ReplyDelete
  7. Pius Jacob amekuwa mfano ule wa kula KUKU NA MAYAI YAKE!!!

    Bendi yetu ya Vijana Jazz Wana Pambamoto chini ya Kiongozi wake Hayati Hemedi Maneti iliwahi kualikwa kwenda kutumbuiza huko Bujumbura-Burundi.

    Kwa kweli walionyeshwa ukarimu mkubwa sana na Wenyeji wao huko ugenini nchi jirani KWA KUCHINJIWA KUKU NA MAYAI YAKE hadi waliporudi Tanzania wakatunga wimbo!

    HIVYO WAO VIJANA JAZZ WANATUELEZA NI NAMNA GANI WALICHINJIWA KUKU N MAYAI YAKE,,,AKU MIMI SIMO ATAELEZA MWANAMUZIKI YEYOTE WA ILIYOKUWA VIJANA JAZZ,,,MSIJE MKANIKABA KAMA MDAU WA KWANZA HAPO JUU.

    Sasa ndugu yetu Pius Jacob huko Nkasi-Shinyanga AMETUKUMBUSHIA WALIVYO STAREHE VIJANA JAZZ WAKIWA BUJUMBURA -BURUNDI KWA KITENDO CHA KULA KUKU NA MAYAI YAKE kwa KUOA WASICHANA WAWILI NDUGU!

    ReplyDelete
  8. Ohooo Pius Jacob una moyo mgumu sana Msukuma wewe!

    Hivi kwa kuzawadia wabinti wawili wa Familia moja, je Mahali ulilipa Kiasi gani kwa wazazi wao?

    ReplyDelete
  9. Ehhh!

    Unawamudu vipi huku wakijijua wao ni ndugu?

    Au umewafanyia Ushirikiana UMEWADUMAZA KIAKILI MPAKA WAMEKUWA MAZEZETA na ukwakamata kwa njia ya ndumba?

    Hivi hao wasichana ndugu hata wivu hawaoneani?

    ReplyDelete
  10. Yaani thamani ya Mwanamke ina dhalilishwa sana kwa Jadi potofu kama hizi!

    Yaani unaloweka dude kako kwa dada mtu usiku kucha usiku huu na usiku unaofuata unalichomoa na kulichomeka kwa mdogo wake?

    Wewe Pius Jacob mshenzi mkubwa na mchafu sana!

    HAYA SIO MAADILI YA MTANZANIA NA KIGEZO CHEMA, NI LAZIMA UFUNGWE SANA ILI IWE FUNDISHO KWA WENGINE!

    ReplyDelete
  11. Hakuna Cheo kingine cha kumpa huyu Pius Jacob kwa kitendo cha Kibazazi alichofanya bali ni kuwa Mpanda Farasi mchunga ng'ombe wa Marekani maarufu kama MARLBORO!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...