MAREHEMU SAMWEL P. KITULA
Ikiwa
ni siku moja imepita Tangu Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Dodoma
kiondokewe na aliye wahi kuwa Mwanafunzi wa Chuo hicho katika Level ya
Diploma 2012/2013 Marehemu Zeinabu J. Kasenga (ODMK -2012/2013)
Simanzi zimezidi kutanda Chuoni hapa baada ya Mwanafunzi Mwingine Bw. Samwel P. Kitula (37)
aliyekuwa akisoma Bachelor Degree in Procurement and Supplies
Management mwaka wa tatu (3) mkondo "A" Kufariki Dunia usiku wa
kuamkia Tarehe 26/12/2013 ( Mnamo saa 8 usiku) katika hospitali ya
Mkoa wa Dodoma (General Hospital).
Kwa mujibu wa Msemaji wa Familia amesema Marehemu alikuwa akisumbuliwa na Matatizo ya Ini mpaka kupelekea Mauti yake.
Kwa
upande wake Rais wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya
Biashara (CBE) Kampasi ya Dodoma Mhe. Remidius M. Emmanuel amesema amepokea taarifa hiyo kwa majonzi makubwa sana na kuwataka wanafunzi
wote kuwa wavumilivu hasa katika kipindi hiki kigumu cha kumpoteza
mwanafunzi mwenzetu.
Rais huyo amewataka wanafunzi kuwa watulivu wakati taratibu mbalimbali zinaendelea na kila kitakachoendelea watafahamishwa kupitia taratibu mbalimbali za mawasiliano hapa chuoni.
Amasema Marehemu amekuwa akiishi na familia yake eneo la Makole karibu kabisa na Lodge ya ELGON, na amemtaka kila mtu kwa nafasi yake kujongea eneo hilo kwa ajili ya kutoa pole kwa Familia ya Marehemu.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...