Jumla ya wahitimu 1225 wanatarajia kupata shahada za uzamili katika programu mbalimbali wakati wa mahafali ya 12 ya Chuo Kikuu Mzumbe, Kampasi ya Dar es Salaam kesho.
Naibu Mkuu Chuo hich kampasi Dar es Salaam, Dkt. Andrew Sulle, wahitimu hao wako katika makundi nane ya programu mbalimbali.
Dkt. Sulle aliwaambia waandishi wa habari kuwa Kati ya hao, 426 watatunukiwa shahada ya uzamili ya biashara-menejimenti ya mashirika; 219 shahada ya sayansi ya uzamili ya uhasibu na fedha; 161 shahada ya sayansi ya uzamili ya ununuzi na ugavi.
Kwa Mujibu wa Naibu Mkuu huyo wa chuo, 52 shahada ya sayansi ya uzamili ya masoko; 33 shahada ya uzamili ya biashara (watendaji wakuu); 212 shahada ya sayansi ya uzamili raslimali watu; 119 shahada ya uzamili ya utawala na watatu shahada ya uzamili ya utawala ya watendaji wakuu.
Naye Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chuo hiyo, Bi. Rainfrida Ngatunga amesema katika taarifa yake kuwa Mahafali haya ya kampasi ya Dar es Salaam yanakuwa ya mwisho katika mwaka huu wa masomo.
“Kama ilivyokuwa desturi yetu mahafali tunayafanya kwa kila kila kampasi peke na baada ya yale ya kampasi kuu Morogoro na Mbeya kesho (leo) tunahitimisha na Dar es Salaam ambayo inatunuku shahada za Uzamili tu,” Ngatunga.
Wakati huo huo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, anatarajia kesho kufungua jengo jipya la ghorofa tano katika kampasi hiyo ya Dar es Salaam.
“Jengo hilo ni moja ya juhudi za kupanua kampasi hiyo na lina ofisi, maktaba mbili za kisasa na ukumbi wa mikutano wenye vifaa vya kisasa” Bi. Ngatunga alisema.
Bi. Ngatunga amesema hatua ya ufunguzi wa jengo hilo inaashiria juhudi za chuo hicho kupanua elimu ya juu Tanzania.Kampasi ya Dar es Salaam ilianzishwa mwaka 2005.
Tokea kipindi hicho kampasi hiyo imekua na kufanikiwa kuwa na shahada zaidi ya 10 za uzamili.
“Katika mwaka wa masomo wa 2013/2014, kampasi hiyo inatarajia kuanzisha shahada mpya ya uzamili ya sayansi ya uongozi na menejimenti,” aliongeza mkurugenzi huyo wa mawasiliano.
Hii itafanya kampasi hiyo kuwa na jumla ya shahada za uzamili 13.
Mwandishi; Si leo bali ni kesho tarehe 20 nami nimo mdau...nakula ze Nondoz! Karibuni sana
ReplyDeleteyes na mimi nipo hiyo kesho mdau
ReplyDelete