Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa 
Bw. Emanuel Mteming'ombe enzi za uhai wake

 Mzee Teming'ombe akilia  kwa  uchungu  kufuatia  kifo  cha kijana wake aliyekuwa katibu  wa CCM mkoa wa  Iringa Emanuel Mteming'ombe aliyefariki usiku wa   kuamkia  leo  katika Hospital ya Rufaa ya  mkoa wa Iringa 

Waombolezaji wakiwa  katika hospital ya rufaa ya mkoa wa Iringa katika maandalizi  ya mwili  wa aliyekuwa katibu wa CCM mkoa wa Iringa  


 Waombolezaji  wakishusha jeneza  la kuuweka mwili wa katibu wa CCM mkoa wa Iringa

Na Francis Godwin, Iringa
KATIBU  wa  chama cha mapinduzi  (CCM) mkoa  wa  Iringa Bw Emanuel Mteming'ombe amefariki  dunia katika hospital  ya  mkoa  wa  Iringa.

Katibu   huyo  alikuwa amelazwa  katika Hospital  ya  mkoa  wa  Iringa   moja akisumbuliwa  kwa ugonjwa athma kabla ya kufariki dunia usiku wa kuamkia leo.
Mwenyekiti  wa  CCM  mkoa wa  Iringa Bi, Jesca Msambatavangu  amethibitisha   juu ya taarifa  hiyo  na  kuwa  taratibu  za mazishi  zinafanywa.
Taarifa zinasema mwili wa Maarehemu  unatarajiwa  kuombewa  katika kanisa la RC Kichangani ama nyumbani kwake Gangilonga mjini Iringa kabla ya  kuondoka mida ya saa 10  jioni kwenda Rujewa, Mbarali,  mkoa  wa Mbeya,  kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika  kesho  saa 5 asubuhi.

Katibu  huyo alifariki dunia majira ya saa 8 hivi  usiku  wa kuamkia leo baada ya kulazwa katika Hospital ya  Rufaa ya mkoa  wa Iringa kwa tatizo  la figo na Athma.

Mungu ailaze  roho  yake mahali pema peponi.
Amina

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...