Basi la Abiria la Kampuni ya Burudani linavyoonekana baada ya kupata ajali mbaya sana leo iliyopelekea kupoteza maisha kwa watu 12 huku wengine zaidi ya 30 wakiwa kwenye hali mbaya.ajali hiyo imetokea leo eneo la Kwaluguru,Kwedizinga  wilayani Handeni,Mkoani Tanga.
WATU 12 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa vibaya baada  ya basi la abiria walilokuwa wakisafiria la Kampuni ya Burudani linalofanya safari zake kati ya Korogwe mkoani Tanga kwenda Jijini Dar es Salaam kuacha njia na kupinduka.

 Ajali hiyo imetokea mapema leo asubuhi majira ya saa 1.30 katika eneo la Kwaluguru,Kwedizinga  wilayani Handeni,Mkoani Tanga.

Akithibitisha kutokea ajali hiyo,Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga,Constantine Massawe alisema kuwa ajali hiyo iliyohusisha gari lenye namba za usajili T 610 ATR aina ya Nissan,imetokea leo na kusababisha vifo vya abiria 12 na wengine zaidi ya 30 wako kwenye hospitali ya Wilaya ya Korogwe,wakiendelea kupatiwa matibabu.

Kamanda Massawe aliendelea kusema kuwa  dereva wa basi hilo ajulikanaye kwa jina la Luta Mpenda(35) ni miongoni mwa watu wanaosadikiwa kufa na kwamba miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya wilaya ya Korogwe ya Magunga.

“Majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya magunga na hali zao bado siyo nzuri sana lakini na miili ya marehemu pia imehifadhiwa magunga”,alisema Kamanda Massawe.

Hata hivyo alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa basi hilo ambapo alipofika kwenye kona ya eneo la Kwalaguru gari lilimshinda na  kupinduka. 
Wakazi wa Wilaya ya Korogwe wakiwa wamefurika kwenye Hospitali ya Magunga walipohifadhiwa marehemu na majeruhi.
Wauguzi wa Hospitali ya Magunga wakiendelea kutoa huduma kwa majeruhi wa ajali hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mrisho Gambo akitokea chumba cha maiti cha Hospitali hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Poleni Sana kwa Ajali hiyo mbaya.
    wow! Ajali nyingi sana juu ya barabara zetu. Hii haikubaliki or is not acceptable. Waaziri wa road & and transportation - uko wapi? na pia owner wa hiyo basi? uko wapi? How come we do not hear from them?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...