Watu wane wamekufa na wengine 63 kujeruhiwa
baada ya Treni ya abiria kuacha reli na kupinduka katika sehemu yenye kona kali
maeneo ya Bronx jijini New York, Marekani, mamlaka zimeeeleza.
Gavana Cuomo amesema marehemu watatu
wamekutwa nje ya treni na mmoja ndani yake, Hakutaja majina kwa kuwa familia
zao bado kujulishwa, na kwamba majeruhi 11 wako mahututi, akiwemo dereva wa
treni hilo.
Msemaji wa Metropolitan Transportation
Authority, Bi Marjorie Anders amesema sehemu hiyo yenye kona kali iko katika
eneo la mwendo mdogo, na kwamba kifaa cha mawasiliano kijulikanacho kama black box kitafafanua treni hio ilikuwa
inasafiri kwa mwendo gani.
Ripota wa Globu ya Jamii aliyekuwa eneo la tukio anafuatilia kujua kama kuna Mtanzania aliyehusika katika ajali hiyo, ikizingatiwa kwamba New York kuna Watanzania wengi wanaoishi jijini humo.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...